Vera Sidika adaiwa kukataa kulipa deni la 5,000 na kumkosea heshima mcheshi Akuku Danger

Kulingana na Akuku Danger, Vera alilipa shilingi 10,000 kabla ya kupokea vifaa alivyoagiza na kuahidi kulipa shilingi elfu tano zilizobaki punde baada ya kuzipokea ila akakaidi ahadi.

Muhtasari

•Kupitia mtandao wa Instagram, Akuku Danger amedai kuwa alikodisha Vera vyombo vya sauti  za kutumika kwenye hafla ya kufichua jinsia ya mtoto ambaye amebeba kwa shilingi 15,000.

•Akuku Danger amesema kuwa kilichomkasirisha zadi sio kukosa kulipwa baki lake ila na madharau ambayo Vera alimfanyia pamoja na timu yake.

Image: INSTAGRAM

Mcheshi Akuku Danger amemkashifu mwanasoshalaiti Vera Sidika kwa kukosa kumlipa deni la shilingi elfu tano.

Kupitia mtandao wa Instagram, Akuku Danger amedai kuwa alikodisha Vera vyombo vya sauti  za kutumika kwenye hafla ya kufichua jinsia ya mtoto ambaye amebeba kwa shilingi 15,000.

Kulingana na Akuku Danger, Vera alilipa shilingi 10,000 kabla ya kupokea vifaa alivyoagiza na kuahidi kulipa shilingi elfu tano zilizobaki punde baada ya kuzipokea ila akakaidi ahadi.

"Baada ya kutimiza niliyofaa kufanya ambapo ilikuwa saa tatu usiku, niliitisha baki langu ila akajifanya hatujui  na akatuma kikundi cha walinzi. marafiki wake walevi na jamaa kwa jina Victor kutufurusha" Akuku Danger alisema.

Alidai kuwa kwa wakati huo wote Vera alikuwa amesimama akijifanya kama kwamba anatumia simu yake.

Akuku Danger amesema kuwa kilichomkasirisha zadi sio kukosa kulipwa baki lake ila na madharau ambayo Vera alimfanyia pamoja na timu yake.

"Naweza ruhusu 5k zizame ila madharau ambayo ulinionyesha pamoja na timu yangu usiku wa jana(Jumamosi)  ndiyo inafanya nifanye haya. Kwa ufupi, hata 10k ulizonilipa zilipotelea. Sasa niko na karisaji  kwani timu yangu inanidai malipo. Unataka nifanyeje?" Akuku Danger aliandika.

Vera alifanya sherehe ya kufichua jinsia ya mwanawe mtarajiwa usiku wa Jumamosi. 

Kwenye hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na wageni waliokuwa wamealikwa, Vera alifichua kuwa anatarajia mtoto wa kike.