- Wanamitandao wazua mdahalo baada ya msanii Rayvanny kupakia picha yake Paula Kajala
Uvumi umekuwa ukiendelea kwa muda sasa kuwa msanii Rayvanny alitema familia yake kwa ajili ya kipusa Paula Kajala ambaye ni mwanawe muigizaji wa Tanzania Fridah Kajala.
Msanii huyo hakujitokeza na kukubali wala kukana uvumi huo.
Kwenye mitandao ya kijamii ya instagram wanamitandao wamezua dhahalo baada ya msanii huyo kupakia picha ya Paula kwa mara ya kwanza tangu uvumi huo kuenea sana.
Baada ya kupakia picha ya Paula kwenye ukurasa wake wa instagram hakuandika chochote, bali mashabiki wake waliotoa hisia tofauti.
Hisia za mashabiki;
prettychrissog: Kufichaa mapenz ni sawaa na kujamba ukiwa kweny majiii, lazmaa juu tutaonaaaπππ
uality__giessel__jewelry: ππππ@therealpaulahkajala dada funga zikaze unapostiw bila caption bado sanaπππ
chrissrobee: Amkeni amkeni wale askari waliomtesa yesu wamerudi ulimwenguni
mwajuma3132: Ata caption kaka unatupia tu π₯±π₯Ί
helleneliasofficial: Happy birthday wifi sisi kama wanyakyusa tunasema TUMEKUPOKEA karibu Tukuyu π
gwickietanza: Uyu mwaisa naye kutudhalilisha jamani π’π’π’π’π’ kha ....no caption Wala nn acha upendeleo Kama wifi aliyepita tunaomba caption mambo ya kibubu bubu no
jojoalimamukeshimana: Wengine wanaposti magari ww unaposti mademuπ
Je kulingana na maono yako wawili hao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi au msanii huyo ni kiki anatafuta?