Wewe ndio sababu kuu yangu na baba yako kubarikiwa-Diana Marua kwa mwanawe Morgan

Muhtasari
  • Diana Marua amwandikia mwanawe Morgan barua ya kipekee
Image: Hisani

Diana Marua mkewe msanii Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesimulia jinsi amekuwa na uhusiano wa karibu na mwanawe Morgan Bahati.

Diana alifichua kwamba mwanawe alipomuita mama hakuwa tayari kwa jukumu hilo, bali anamshukuru Mungu kwani ndiye sababu kuu yao kuwa na baraka maishani mwao.

"Wakati mwingine mimi huketi chini na kumuuliza Mungu kwanini nimebarikiwa hata wakati sistahili ... Halafu namsikia akinong'ona, "ulimkubali kwa moyo wote kama mtoto wako."

@Morgan_bahati ulikuwa wa kwanza kuniita mama hata wakati sikuwa tayari kuigiza jukumu hilo.

Nakumbuka siku moja ulirudi nyumbani kutoka kucheza kisha ukaniuliza ... "Shangazi Dee, marafiki wa mbona wangu wanauliza mbona naita Baba-Baba na wewe Nakuita Aunty na Sio Mama?"

Maneno hayo yalinitoboa moyoni mwangu na niliweza kuona ukweli katika macho yako ya wewe kutaka mtu amwite Mama

Nilikuwa katika maisha yako hapo na milele .... Nilipenda Baba yako na kila kitu alikuwa nacho ikiwa ni pamoja na wewe na familia yake.

Nilitaka uniite "Mama" wakati ulikuwa sawa, kwa wakati wako mwenyewe. Siku hii, ulikuja na kuniuliza hiyo ... nilikuambia uniite Mama ikiwa uko sawa nayo na haujawahi kuniita "Aunty Dee" tena hata kwa makosa."Diana aliandika.

Diana alisema kwamba maneno hayawezi elez jinsi anavyompenda mwanawe.

"Ninakupenda kama mtoto wangu wa kwanza, zaidi ya maneno hayawezi kuelezea. Ninamshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote. Wewe ni moja ya sababu kubwa kwa nini mimi na Baba yako tumebarikiwa.

Asante kwa kuniita Mummy. Umekuwa mvulana mkubwa sasa, karibu kijana na unanishangaza na IQ yako ya kila siku. Upendeleo na Baraka Zake Zikupate Siku Zote za Maisha Yako."