Niliona umepata mtu 'handsome' nialike kwenye harusi-Bahati kwa Vyette Obura

Muhtasari
  • Bahati amwandikia mama wa mtoto wake Yvette Obura
Bahati
Bahati
Image: Instagram

Msanii Bahti, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, amemwamndikia mama wa mtoto wake Yvette Obura ujumbe akimuomba msamaha.

Je msamaha ni wa nini?

Kulingana na msanii huyo aliwaficha wawili hao kwa zaidi wa miaka miwili, jambo ambalo halikumfurahisha.

"Ulikuwa wakati nafika kileleni kama msanii wa nyimbo za injili, punde baada ya kupata tuzo la Groove la msanii bora wa kiume na tuzo la AFRIMMA. Wakati huo nilikuwa nahukumiwa sana, najua mnanielewa. Niliishia kuwa mnafiki badala ya kujivunia damu yangu" Bahati aliandika.

Mapema mwaka huu, Yvette alikuwa na mpenzi ambaye baadaye waliachana, lakini ni kama msanii huyo hajui hilo.

Kwenye ujumbe wake alimpongeza Mama Mueni kwa kumpata mchumba, huku akisisitiza kwamba angefurahi sana kama angemualika kwenye harusi yake.

"Pia nilisoma kwenye blogs kuwa umepata mtu handsome. Tafadhali ningefurahia kualikwa kwenye harusi yako. Mungu abariki maisha yako, safari na yote unayoyafanya" Bahati alimwandikia Yvette.

Zaidi ya yote Bahati alimshukuru Yvette kwa kuchagua amani maishani mwake licha ya yote alipitia mikononi mwake.