WAMEWEZA, HAWAJAWEZA?

(+Video) Heartbreak! Willy Paul na Alaine washirikiana kutoa kibao kingine

Mwaka wa 2017 wawili hao walishirikiana kutengeneza kibao 'I do' ambacho kilivuma sana huku kikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 24 kufikia sasa.

Muhtasari

•Heartbreak' (Kuvunjwa moyo) ni wimbo ambao unazungumzia masaibu wanayoyapitia wanandoa.

Image: HISANI

Miaka minne baada ya kutoa wimbo pamoja, Willy Paul na Alaine wameshirikiana kwenye kibao kingine.

Willy Paul na mwanadada huyo kutoka Jamaica mwenye sauti ya kupendeza kweli wameshirikiana kuimba wimbo 'Heartbreak' ambao uliwachiliwa Jumatano asubuhi.

Mwaka wa 2017 wawili hao walishirikiana kutengeneza kibao 'I do' ambacho  kilivuma sana huku kikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 24 kufikia sasa.

Wimbo 'I do' ulisababisha uvumi kuwa huenda wawili hao walikuwa wanachumbiana.

Miaka miwili baadae walishirikiana kwenye wimbo mwingine kwa jina 'Shado Mado'.

'Heartbreak' (Kuvunjwa moyo) ni wimbo ambao unazungumzia masaibu wanayoyapitia wanandoa.

Unagusia mambo ya kawaida katika ndoa na mashida  ambayo wanandoa hupitia kwenye mahusiano yao.

Tazama hapa;-

#WillyPaul #Alaine #heartbreak this song touches on real life issues. Talks about marriages and what normal couples go through.

Je, kibao kimeweza au la?