ALIMWANDIKIA OMBI LA MSAMAHA INSTAGRAM

'Nilikusamehe kitambo kwa sababu ya binti wetu' Obura amjibu Bahati baada ya kuomba msamaha

Yvette alimwambia Bahati kuwa alimsamehe ili bintiye aweze kukua katika mazingira yenye amani na upendo.

Muhtasari

•Siku ya Jumanne,Bahati alitumia mtandao wa Instagram kumuomba msamaha Yvette na binti yake Mueni Bahati kwa kuwaficha kutoka kwa watu kwa kipindi cha miaka miwili wakati alikuwa anaanza kupata umaarufu mkubwa.

•Bi Obura alimshukuru Bahati kwa kumuomba msamaha hadharani  na akamuombea baraka tele.

Image: INSTAGRAM

"Wewe ni baba mzuri kwa Mueni na naamini hilo ndo muhimu" 

Ndio ujumbe wa bi Yvette Obura kwa mwanamuziki Bahati baada yake kuandika ujumbe mrefu akimuomba msamaha pamoja na bintiye.

Siku ya Jumanne,Bahati alitumia mtandao wa Instagram kumuomba msamaha Yvette na binti yake Mueni Bahati kwa kuwaficha kutoka kwa watu kwa kipindi cha miaka miwili wakati alikuwa anaanza kupata umaarufu mkubwa.

Bahati alieleza kuwa kuhukumiwa sana na Wakenya kulimfanya kugeuka kuwa mnafiki na kutojivunia damu yake wakati bintiye alizaliwa.

"Ulikuwa wakati nafika kileleni kama msanii wa nyimbo za injili, punde baada ya kupata tuzo la Groove la msanii bora wa kiume na tuzo la AFRIMMA. Wakati huo nilikuwa nahukumiwa sana, najua mnanielewa. Niliishia kuwa mnafiki badala ya kujivunia damu yangu" Bahati aliandika.

Akijibu ombi la Bahati, Yvette alimwambia mwanamuziki huyo kuwa alimsamehe kitambo  sio kwa sababu yake mwenyewe ila kwa minajili ya binti yao Mueni.

Yvette alimwambia Bahati kuwa alimsamehe ili bintiye aweze kukua katika mazingira yenye amani na upendo.

"Nilikusamehe kitambo sana. Sio kwa minajili yangu ila kwa sababu ya Mueni. Ili aweze kukua katika mazingira yenye amani na upendo" Yvette alimjibu Bahati.

Bi Obura alimshukuru Bahati kwa kumuomba msamaha hadharani  na akamuombea baraka tele.

Kwa sasa Bahati amemuoa mwanadada mrembo kwa jina Diana Marua ambaye wamefanikiwa kuwa na watoto wawili pamoja; Heaven Bahati na Majesty Bahati.  

Wawili hao pia wamepanga mtoto mmoja anayejulikana kama Morgan Bahati.

Bahati na Obura wameendelea kushirikiana vyema katika ulezi wa binti yao Mueni Bahati.