SIKU YA KUADHIMISHA 'EMOJIS'

'Emojis' maarufu zaidi miongoni mwa Wakenya -Utafiti

Emoji tatu za chakula maarufu zaidi nchini Kenya ni ile ya keki mzima, keki nusu na ile ya tunda la tango.

Muhtasari

•Dunia inapoadhimisha siku hiyo, mtandao wa Facebook umetangaza matokeo ya utafiti wa emoji zinazotumiwa sana na Wakenya.

•Hata hivyo, watu wenye umri wa miaka zaidi ya 45 walitumia sana emoji ya mikono mbili iliyolaliana ambayo huashiria shukrani ama maombi.

Image: HISANI

Ifikapo kesho (Julai 17) dunia itaadhimisha siku ya 'emojis'. 

Hizi ni ishara za simu ambazo hutumika kuonyesha  hisia za mtu anapokuwa kwenye mazungumzo ya kutumiana jumbe na mwingine.

Dunia inapoadhimisha siku hiyo, mtandao wa Facebook umetangaza matokeo ya utafiti wa emoji zinazotumiwa sana na Wakenya.

Utafiti huo ulifanywa kati ya mwezi wa Aprili na mwezi wa Julai.

Imebainika kuwa emoji zilizotumiwa na sana miongoni mwa Wakenya ni ile ya ishara ya moyo (Upendo) na za kicheko.

Image: HISANI

Emoji hizo zilikuwa maarufu miongoni mwa jinsia zote mbili na makundi yote ya umri.

Image: HISANI
Image: HISANI

Hata hivyo, watu wenye umri wa miaka zaidi ya 45 walitumia sana emoji ya mikono mbili iliyolaliana ambayo huashiria shukrani ama maombi.

Image: HISANI

Emoji tatu za chakula maarufu zaidi nchini Kenya ni ile ya keki mzima, keki nusu na ile ya tunda la tango.