Staa wa Benga ajitoa uhai kwa kujizamisha ndani ya mto juu ya deni la 700,000

"Nikitoweka msijisumbue kunitafuta sana kwani nitakuwa mtoni Sagana. Msongo wa mawazo unaniua." Aliandika Wanjaro Jr kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

Muhtasari

•Mwili wa Wanjaro ambaye alitoweka kutoka nyumbani kwake siku ya Jumanne ulipatikana Jumamosi ukiwa umeelea kwenye bwawa la Masinga lililo maeneo ya Mbeere.

•Inaaminika kuwa Wanjaro aliamua kujitoa uhai kufuatia msongo wa mawazo uliotokana na deni la 700,000 ambalo alikuwa ameshindwa kulipa.

•Wanjaro Jr ni ndugu wa marehemu Mwalimu George Wanjaro ambaye aliaga mwaka wa 2007 baada ya kuheshimika sana kwenye sekta ya muziki wa Kikuyu.

Bwawa la Masinga alikopatikana Wanjaro Jr
Bwawa la Masinga alikopatikana Wanjaro Jr
Image: HISANI

Mwanamuziki wa nyimbo za Kikuyu Edward Irungu Njaro almaarufu kama Wanjaro Juniour anaripotiwa kujitoa uhai kwa kujizamisha ndani ya mto Sagana.

Mwili wa Wanjaro ambaye alitoweka kutoka nyumbani kwake siku ya Jumanne ulipatikana Jumamosi ukiwa umeelea kwenye bwawa la Masinga lililo maeneo ya Mbeere.

Inaaminika kuwa Wanjaro aliamua kujitoa uhai kufuatia msongo wa mawazo uliotokana na deni la 700,000 ambalo alikuwa ameshindwa kulipa.

Mwanamuziki huyo alikuwa ameandika ujumbe  akiarifu familia na marafiki mahali wangepata mwili wake.

"Nikitoweka msijisumbue kunitafuta  sana kwani  nitakuwa mtoni Sagana. Msongo wa mawazo unaniua." Aliandika Wanjaro Jr kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

Familia ya marehemu ilikuwa imetoa ombi kusaidiwa kumtafuta baada yake kuacha ujumbe huo. Gari lake lilipatikana likiwa limeachwa kwenye daraja moja la kuvukia mto Sagana.

Wanjaro Jr ni ndugu wa marehemu Mwalimu George Wanjaro ambaye aliaga mwaka wa 2007 baada ya kuheshimika sana kwenye sekta ya muziki wa Kikuyu.