'Naona umekuwa prefect wa Mungu,'Nicah the Queen amjibu shabiki aliyekejeli mavazi yake

Muhtasari
  • Nicah the Queen amjibu shabiki aliyekejeli mavazi yake
Nicah the Queen
Image: Studio

Msanii wanyimbo za Injili Veronica Wanja almaarufu Nicah The Queen ameshambuliwa tena mitandaoni kwa sababu ya mavazi yake wakati akihudhuria ibada ya kanisa.

Kupita kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwimbaji alishiriki kipande cha video fupi akikumbatiana na mshirika mwingine wa kanisa.

Kama mashabiki wake wengi walithamini kukaribishwa kwake, wengine walizingatia chaguo lake la mavi wake.

Sio mara ya kwanza msanii huyo ukejeliwa au kushambuliwa mitandaoni kwa ajili ya mavazi yake akiwa kanisani.

Nicah hakukimya bali alimpa jibu mmoja wa mashabiki wake ambalo liliwanyamazisha wengi ambao walimshambulia.

i_am_offela :dressing decently in the house of the LORD is enough respect plizz," Shabiki huyo alimwambia Nicah.

Naye alikuwa na haya ya kumjibu;

"@i_am_offela juu unaona niko uchi.....naona umekuwa prefect wa mungu! Peleka opinion yako hukooo mbali na mimi

@i_am_offela kwa sababu nimechoka na watu kama nyinyi!! badala ya kusafisha mioyo yenu mko makini sana mkisema jinsi watu wanapaswa kuvalia nguo katika maisha yao.Nyinyi ni wale watu husengenya watu kanisani na kuwafanya waende!Wacha, kama huna lolote la kufanya nenda ukaleta mtu mmoja kanisani," Alimjibu Nicah.

Je kuna mavazi unapaswa kuvalia kanisani?