Ishara ya mapenzi: Vanessa Mdee achorwa jina la mpenzi wake Rotimi

Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2019 baada ya Vanessa kutengana na aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi kirefu, mwanamuziki Jux.

Muhtasari

•Mdee alifichua hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kupakia picha iliyoonyesha tatoo yake mpya ambayo ni jina Rotimi, jina ambalo mpenzi wake anatumia kwenye usanii wake.

•Hivi karibuni mwanamuziki huyo alikanusha madai kuwa  amejifungua mtoto wao wa kwanza  na mpenzi wake.

Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki kutoka Tanzania Vanessa Hau Mdee ameonyesha upendo mkubwa anao kwa kipenzi chake Olurotimi Akinosho almaarufu kama Rotimi kwa kuchorwa tatoo ya jina lake.

Mdee alifichua hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kupakia picha iliyoonyesha tatoo yake mpya ambayo ni jina Rotimi, jina ambalo mpenzi wake anatumia kwenye usanii wake.

Rotimi ni mwigizaji, mwanamuziki na mwanamitindo mzaliwa wa Marekani kwa wazazi kutoka Nigeria.

Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2019 baada ya Vanessa kutengana na aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi kirefu, mwanamuziki Jux.

Hivi karibuni mwanamuziki huyo alikanusha madai kuwa  amejifungua mtoto wao wa kwanza  na mpenzi wake.

"Sina mtoto mimi. Mnampa  mamangu wasiwasi. Mama watu ako zake Arusha mnaanza kumpa wasiwasi kwamba nimezaa.Ebu niwaulizeni, nani amemwambia." Alisema Mdee kupitia mtandao wa Instagram.

Mdee sio mwanamuziki wa kwanza kutoka Bongo ambaye amewahi kuchorwa jina la mpenzi wake.

Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake mwigizaji  Frida Kajala waliwahi kuchora herufi ya kwanza ya mwingine kwenye upande wa shingo zao .

Fridah Kajala na Harmonize
Fridah Kajala na Harmonize
Image: HISANI

Hata hivyo, Harmonize alifuta tatoo hiyo mwezi Aprili huku Fridah akificha yake pia wiki iliyopita.