'Bibi akiuliza maswali sitaki kujibu nashika rosari nalala' Atwoli ataja siri ya kuzuia mzozo kwa ndoa

Atwoli amesema kuwa wanandoa wakiweka Mungu mbele na kuomba sana ndoa itastawi.

Muhtasari

•"Sisi ni Wakatoliki, na sisi huwa na rosari ile wakati usingizi umekosa nashika rosari naomba, uliza Maria ... Maria akiniuliza ile maswali yenye sitaki kujibu nashika rosari, naomba,  nalala badala ya kushindana na yeye" Atwoli alisema.

Image: HISANI

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli ameshauri wanandoa kutumia maombi kama ngao ya kuzuia mzozo kwenye ndoa.

Atwoli amesema kuwa siri ya kutatua malumbano baina yake na mkewe Mary Kilobi ni kupitia maombi.

"Sisi ni Wakatoliki, na sisi huwa na rosari. Ile wakati usingizi imepotea nashika rosari naomba, uliza hata Maria ... Maria akiniuliza ile maswali yenye sitaki kujibu nashika rosari, naomba,  nalala badala ya kushindana na yeye" Atwoli alisema.

Atwoli alisema hayo wakati alikuwa  akipatia ushauri wanandoa ambao walikuwa wakifunga pingu za maisha. 

Atwoli alisesema kuwa wanandoa wakiweka Mungu mbele na kuomba sana ndoa itastawi.

Atwoli na Kilobi walifunga ndoa mwaka wa 2018. Hivi majuzi wawili hao waliandamana kuelekea  Watamu, Kilifi kusherehekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Kilobi.