Watu waache kutafuta kiki,'King Kaka asema baada ya kibao chake na Otile Brown kutolewa kwenye youtube

Muhtasari
  • KIng Kaka awaka moto baada ya kibao chake na Otile Brown kutolewa youtube
King Kakak na Otile Brown
Image: hisani

Rapa Kennedy Ombima, anayefahamika zaidi kwa jina lake la jukwaani King Kaka kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaita wasanii chipukizi waache kutumia madai ya uongo ya hakimiliki ili kupata kiki.

Wimbo uliopewa jina la 'Fight' tayari ulikuwa umepokea watazamaji zaidi ya nusu milioni kwenye YouTube; lakini imeondolewa tangu wakati huo kwa madai ya hakimiliki.

Akiwa amejawa na hasira, King Kaka aliandika kwenye Instagram yake;

"Hizi Copyright Claim zimekuwa mingi.watu wanapaswa kuacha kutafuta kiki na kufanya muziki.kibao ambacho tulifanya kuanzia mwanzoni na @otilebrown in a studio tena iko na kesi," Aliandika Kaka.

Madai hayo yanakuja siku chache baada ya wimbo wa Krispah uliopewa jina la 'Ndovu Ni Kuu' akimshirikisha Khaligraph Jones na Boutross kuondolewa kwenye YouTube kutokana na masuala ya hakimiliki.

Msanii kwa jina Dexter alidai kuwa wimbo huo ulikuwa umechukua sampuli ya muziki wake. Kinyume chake, Krispah alisema vinginevyo, akisema kwamba Dexter, ambaye aliripoti wimbo huo, alikuwa miongoni mwa wafanyikazi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta ambao walikuwa katika mikono yao kuuvuta wimbo huo.