'Familia yangu wameshuhudia ukarimu wako,'Msanii Akothee azidi kumlimbikizia sifa baby daddy wake

Muhtasari
  • Msanii Akothee azidi kumlimbikizia sifa baby daddy wake
Akothee
Image: hisani

Akothee almaarufu kama Madam Boss ni mama mwenye furaha baada ya kuwapokea wanawe wawili Prince Ojwang na Prince Oyoo nchini kutoka Ufaransa.

Wawili hao walitua katika uwanja wa ndege wa JKIA usiku wakiandamana na baba mzazi wa Oyoo ajulikanaye kama Dominic na ambaye wanaishi naye.

Akothee ambaye alikuwa ameandamana na binti wake wawili Rue Baby na Vesha Okello kuwalaki alionekana mwenye bashasha si haba kuwaona wanawe baada ya kipindi kirefu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee amemlimbkizia sifa baby Daddy wake tena huku akimshukuru kwa kukaa naye na kumuelewa.

"Nikupeleke KWA mamangu na babangu ,wakuombee mola, KWA kunitunza Mimi pamoja na wanangu🙏

👉Familia yangu , Wameshuhudia ukarimu wako wakiwa bado wako hai, sisi kama familia tunakushukuru KWA kumvumilia kichaa chetu Akothee,twajua amekukosea KWA saaaanaaaa Ila wampenda vivyo hivyo," Aliandika Akothee.