Lala salama!Mbosso aomboleza kifo cha msanii mwenzake

Muhtasari
  • Mbosso aomboleza kifo cha msanii mwenzake
  • Alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Wananyamala jijini Dar Es Salaam
  • Mwanachama wa bendi alifichua kwamba marehemu alikuwa na shida za shinikizo la damu
  • Mwaka jana, alikuwa amesafiri kwenda India kwa matibabu ya moyo lakini bado haijajulikana ni nini kilimuua
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n
66855938_1220357588125307_5681176959875639446_n

Waziri Ally Kissinger, mwanzilishi wa bendi maarufu ya Kitanzania Kilimanjaro Band maarufu kwa jina la Wana Njenje alifariki jana usiku.

Alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Wananyamala jijini Dar Es Salaam.

Mwanachama wa bendi alifichua kwamba marehemu alikuwa na shida za shinikizo la damu.

Mwaka jana, alikuwa amesafiri kwenda India kwa matibabu ya moyo lakini bado haijajulikana ni nini kilimuua.

Kupitia kwenye ukurasa wa msanii wa bongi,Mbosso alimuomboleza mwendazake, na kufichua jinsi walikuwa watoe kibao kipya pamoja.

"Daah !! Mzee Wangu Waziri Njenje ..😭 .., Tulifanya wimbo wetu Salama, Tukasafiri Mpaka Tanga na Tukashoot Video Yetu Salama Kabisa na Hivi Juzi tu hapa Tumeongea kwa Furaha kabisa tukiwa tunapanga kutoa Video Ya Wimbo Wetu #Tulizana Leo Umenda Baba .. " Daaah ..

Mwenyezi Mungu Akupe Kauli Thabiti Mzee Wangu , Malaika wa heri Walipambe Kabuli lako Baba 🤲

"Innalillah Wainnailah Raajuun "Hakika Ya Sisi ni Wamwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea 🙏," Aliomboleza Mbosso.

Bendi ya Kilimanjaro iliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita huko Tanga, Tanzania.