'Nitangoja sheria ichukue mkondo wake,niombeeni,'Ringtone azungumza

Muhtasari
  • Hatimaye msanii Ringtone azungumza baada ya kuchapwa
  • Kupitia kwenye Instagram alishiriki video ambapo, Apoko amewashukuru mashabiki wake na madaktari kwa kumtakia afya njema.

ringtone apoko
ringtone apoko

Mwimbaji mashuhuri Ringtone Apoko amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kugombana kwake na mwanablogu Robert Alai.

Kupitia kwenye Instagram alishiriki video ambapo, Apoko amewashukuru mashabiki wake na madaktari kwa kumtakia afya njema.

Alifichua kwamba alikuwa ametoka nje ya hospitali ya Kenyatta ambapo alitibiwa baada ya kuchukua p3.

"Nataka kuwashukuru Wakenya wote ambao waliniombea baada ya shambulio na pia nataka kuwashukuru madaktari wa hospitali ya Kenyatta ambao walinitibu Nataka tu mashabiki waendelee kuniombea, "alisema.

Pia amesema ataendelea kuchukua dawa na kifichua kwamba ataziruhusu sheria ziamue kati ya makabiliano yake na Robert Alai.

Mwimbaji huyo anaonekana na bandeji kwenye uso na pia mkono wake wa kulia unaonekana kuumizwa kama matokeo ya ugomvi.

"Nitangoja sheria ichukue mkondo wake,"

Vita vyao vilitokea siku ya Ijumaa, ambapo ilisababisha mwanablogu Alai kukamatwa kwa madai ya kumshambulia msanii huyo.