'Tunakushukuru papa,' Soma ujumbe wake Zari Hassan kwa baba ya watoto wake Diamond

Muhtasari
  • Soma ujumbe wake Zari Hassan kwa baba ya watoto wake Diamond
Image: Hisani

Zari the boss lady ndiye alikuwa mwanamke wa kwanza katika maisha ya Diamond ambaye walibarikiwa na watoto pamoja.

Kabla ya Diamond kuchumbiana  na Zari, Diamond alikuwa akichumbiana na mwanamitindo bora wa Tanzania Wema Sepetu. Hata hivyo Wema alijaribukupata ujauzito wake Diamond lakini nguvu zake ziliambulia patupu.

Watu wengi walikuwa wamesema kwamba labda Diamond alikuwa na maswala ya uzazi.

Walakini Zari alithibitishia Ulimwengu kuwa  makosa alikuwa mwanamke wa kwanza katika maisha ya Diamond baada ya kubarikiwa na kifungua mimba Princee Tiffah.

Diamond na Zari walipendana sana .

Leo Zari ameamua kuposti picha ya kifamilia na Diamond na Zari ametoa maoni kuwa anamthamini sana Diamond akiwa mtu wa familia.

Huu ni ushahidi halisi kwamba upendo wa kweli husamehe na hauzingatii matendo mabaya.

"Inachukua tu jasiri kugeuka na kufanya jambo sahihi. Tabasamu kwenye @princess_tiffah & @princenillan hazina bei. Tunakushukuru wewe papa 🙏," Aliandika Zari.

Je kuna uwezekano kwamba wawili hao wanweza rudiana?