Akothee ampongeza mchekeshaji YY kwa kumjengea mama yake

Muhtasari
  • Akothee ampongeza mchekeshaji YY kwa kumjengea mama yake
  • YY ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipindi cha Churchill Show alitangaza mafanikio hayo kwenye ukurasa wa Instagram
Image: INSTAGRAM//YY COMEDIAN

Mcheshi Oliver Otieno almaarufu kama YY anajivunia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mama yake.

YY ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipindi cha Churchill Show alitangaza mafanikio hayo kwenye ukurasa wa Instagram.

Msanii huyo alipakia picha mbili ya kwanza akionyesha hali duni ambayo mamake alikuwa akiishi kisha ya pili ikionyesha nyumba maridadi aliyomjengea mamake.

"Kutoka kwa mtoto hadi kwa mama ,, (Kitu ambacho hata watu mashuhuri sana. Kamwe hawajafanya kwa wazazi wao πŸ’ͺπŸ™

Hata Mungu Aliko Nina hakika amesimama, Yy una miaka mingapi? Wanaume katika umri wako wanafurahia maisha mjini. Ja SDA, kwanini usitumie pesa hii huko Dubai (baridi na marafiki zangu!) πŸ™

Mchakato gani wa kufikiria, zawadi ikiwa mwana kwa mama. Wanaume wanaendesha magari makubwa jijini wakiwa na maarifa machache sana juu ya mahali ambapo wazazi wanalala husahau juu ya kile wazazi wao hula. Omera @yycomedian umecheza kama Mwanaume. Natasnia ni ngumu," Aliandika Akothee.

Tofauti na wasanii wengine ambao hupendelea kuambatanisha tangazo la mafanikio kama hayo na jumbe refu, YY hakuwa na maneno mengi ya kuwaambia mashabiki ila tu kumwambia mamaye jinsi anavyompenda.