'Tabia za Wakenya' Raila Odinga apendezwa na kibao cha gengetone cha Mejja

Amesifia sana ubunifu wa wasanii wa Kenya.

Muhtasari

•Mgombeajii huyo wa kiti cha urais ameonekana kupendezwa na kibao cha Mejja 'Tabia za Wakenya'.

•Kupitia mtandao wake wa Twitter Raila alisema kuwa alisikiza maneno ya kibao hicho mahali asubuhi na akakubaliana nayo kuwa ya kweli.

Image: HISANI

Ni dhahiri kuwa aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga ni shabiki wa nyimbo aina ya Gengetone baada ya ujumbe aliochapisha mitandaoni mapema siku ya Jumanne.

Mgombeajii huyo wa kiti cha urais ameonekana kupendezwa na kibao cha Mejja 'Tabia za Wakenya' ambacho kiliondolewa kwenye mtandao wa YouTube mwezi uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Raila amesema kuwa alisikiza  kibao hicho mahali asubuhi na akakubaliana na maneno yake.

"Kibao cha Mejja 'Tabia za Wakenya'  kilichezwa mahali leo asubuhi na kikanifanya kutafakari kumbe ni kweli.!" Raila alisema.

Raila alipendezwa zaidi na mstari kwenye wimbo huo unaosema, "Masaa na Mkenya atachelewa sana. Lakini sherehe tunafika mapema,, tena sana na tunateta umetuweka"

Kulingana na Raila, maneno ya wimbo huo  ni ya kweli kabisa.

Mwanasiasa huyo amesifia sana ubunifu wa wasanii wa Kenya.

Ujumbe huo uliwashangaza wanamitandao wengi kuona kuwa kinara huyo wa ODM na umri wake mkubwa aliweza kuskiza maneno ya wimbo huo licha ya dhana kubwa miongoni mwa wanajamii kuwa nyimbo za gengetone huskizwa na vijana wenye umri mdogo tu.

Kibao 'Tabia za Wakenya' kiliondolewa kwenye mtandao wa YouTube mwezi uliopita kwa utata wa hatimiliki. Hata hivyo bado kinaendelea kuchezwa kote nchini