'Instagram ni ofisi yangu' Vera akosoa wanaomkashifu kwa kupakia picha za ujauzito mitandaoni

Mwanasoshalaiti huyo amedai kuwa hata watu walio kwenye taaluma zingine huenda kazini wakiwa wajawazito.

Muhtasari

•Vera amesema kuwa kuwa mtandao wa Instagram ni moja ya ofisi za watu mashuhuri na kudai kuwa ataendelea kupakia picha zake kama ilivyokuwa kawaida yake hapo awali

•Alisema kuwa alishangazwa mbona watu walikuwa wakikasirika kumuona akipakia picha mitandaoni ilhali wao bado wanaenda kazini, kanisani na mahali kwingineko kila siku

VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amewakosoa watu wanaomkashifu kwa kupakia picha za ujauzito wake mitandaoni.

Vera amesema kuwa kuwa mtandao wa Instagram ni moja ya ofisi za watu mashuhuri na kudai kuwa ataendelea kupakia picha zake kama ilivyokuwa kawaida yake hapo awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanasoshalaiti huyo amedai kuwa hata watu walio kwenye taaluma zingine huenda kazini wakiwa wajawazito.

"Sijui wanatarajia tuvae nguo kubwa ile tufiche tumbo, ama tuondoe ujauzito kwa picha, ama tupakie picha baada ya miezi tisa kwa sababu inaudhi watu. Jambo la kushangaza nikuwa wao wanapokuwa wajawazito bado wataenda kazini kila siku hadi ujauzito ufikishe miezi 7 hadi 9 kwa wengine. Lakini hawataki mimi niendelee kupakia picha Instagram" Vera alisema.

"Ninapopata kazi za kutumbuiza watu, oh tulia, wacha kuranda randa. Oh, hiyo sio nzuri kwa mtoto. Oh, usiende mahali kuna watu wengi. Wanataka nijifungie kwa nyumba , nisipakie chochote na nisifanye kazi kwa miezi tisa kama kwamba watalipa bili mtoto akija" Aliendelea kusema.

Alisema kuwa alishangazwa mbona watu walikuwa wakikasirika kumuona akipakia picha mitandaoni ilhali wao bado wanaenda kazini, kanisani na mahali kwingineko kila siku.