Akothee adai kuwa siku atafariki angependa wanawe na Nelly Oaks pekee wawe kando yake

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwa sasa anataka tu kuwa naye Oaks peke yake na angetamani sana awe kando yake iwapo atajifungua tena.

Muhtasari

•Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee amesema kuwa siku ya kifo chake itimiapo basi ataotaka wawe kando ya mauti yake ni watoto wake na anayeonekana kuwa mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks.

•Akothee amesema kuwa Oaks amekuwepo katika nyakati ambazo amekuwa akipitia magumu

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee amesema kuwa siku ya kifo chake itimiapo basi ataotaka wawe kando ya mauti yake ni watoto wake na anayeonekana kuwa mpenzi wake wa sasa Nelly Oaks.

Madam Boss  ambaye matendo yake ya hivi karibuni kwenye mitandao yameashiria kuwa huenda wanachumbiana na mwanaume huyo aliyekuwa meneja wake ameendelea kumbubujikia sifa si haba.

"Siku moja, kama marehemu anaweza kuona basi kando na watoto wangu mtu mwingine ambaye ningependa kuona kando ya kitanda changu  cha mauti ni Nelly Oaks" Akothee alisema.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Akothee amesema kuwa Oaks amekuwepo katika nyakati ambazo amekuwa akipitia magumu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kwa sasa anataka tu kuwa naye Oaks peke yake na angetamani sana awe kando yake iwapo atajifungua tena.

"Mtu pekee ambaye natamani kuwa naye kwa sasa na mwanaume ambaye nataka awe kando yangu nitakapokuwa kwenye wadi ya kujifungua, Nelly Oaks, Hamjui tunayoyajua,. Jamaa huyu amekuwepo wakati nilikuwa nimeishiwa na nguvu, wakati nilikuwa nimeishiwa kiroho  na kihisia" Akothee alisema.

Mama huyo wa watoto watano amepakia picha wakiwa na Oaks kwenye wadi na kusema kuwa picha ile ilipigwa wakati alikuwa na mongo wa mawazo.

Amesema kuwa Oaks alimsaidia sana kupambana na hali hiyo na hapo ndipo alifanya maamuzi ya kujiimarisha.

Siku za hivi karibuni mwanamuziki huyo amekuwa akipakia picha  na video zake wakiwa pamoja na Bw Oaks kwenye mtandao wa Instagram na kuziambatanisha na jumbe zenye kuashiria hisia za mapenzi na kuibua mdahalo mkubwa mitandaoni ila kwa sasa ameamua kuweka wazi kuwa ni kweli wanachumbiana.

Hivi majuzi Akothee alidai kuwa anampenda Oaks hadi kifo na anaamini kuwa pia yeye anampenda.

"Mapenzi ni kitu nzuri sana. Yeye ndiye mwanaume aliye maishani mwangu kwa sasa. Wengine ni wa awali na waliacha vitu ambavyo tunagawana. Kwa sasa keki ni yake na yake peke yake. Acha kusukuma maisha yako ukutani. Nelly Oaks yumo maishani mwangu sasa"Akothee alisema.

Msanii huyo pia alikiri kuwa alikuwa ameacha manyumba yake makubwa na kuhamia kwa Oaks.

"Kufeli kwa mahusiano yangu ya hapo awali hakumaanishi kuwa sitawahi kuwa na mchumba" Alisema.