Nilimpata mume wangu kwa kichaka na mpango wake wa kando wakifanya tendo la ndoa-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi alimpata mumewe na mpango wake wa kando
sad woman
sad woman

Ni vituko na mambo ambayo watu na wanawake wengi hupitia wakiwa kwenye ndoa, na kuyavumilia yote huku baadhi yao wakikata tamaa ya kuwa kwenye ndoa.

Mwanamke mmoja waliwaacha mashabiki wa radiojambo, midomo wazi baada ya kukiri jinsi alivyompata mumewe na mpango wake wa kando.

Kulingana na mwanamke huyo alidai kwamba alimpata mumewe na mpango wake wa kando wakiwa kwa kichaka huku wakifanya tendo la ndoa.

"Niligundua kwamba mume wangu ana mpango wa kando baada ya kubadili tabia zake, nilisikia fununu kwamba huwa wanapatana kwa kichaka, nilienda siku moja na kumpata na mpango wake wa kando wakifanya tendo la ndoa

Aliponiona hakushtuka lakini alinizamba kofi kwa sababu ya kumfuata,nilipofika nyumbani pia alinipa kichapo cha mbwa, " Alisimulia mwanamke huyo.

Je Ushawahi mpata mpenzi wako na mpango wa kando, au ushawahi patwa na ulifanya nini baada ya kufumaniwa?