Uongo mkubwa wa kizazi hiki ni mitandao ya kijamii-Robert Burale

Muhtasari
  • Robert Burale asema haya kuhusu mitandao ya kijamii
  • Robert Burale amewashauri Wakenya jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa njia ipasayo, ili wasije kujuta baadaye
  • Kulingana na Burale mitandao ya kijamii ni zana nzuri ikiwa inatumiwa vizuri lakini pia ni zana mbaya wakati inatumiwa vibaya
Robert Burale
Robert Burale

Robert Burale amewashauri Wakenya jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa njia ipasayo, ili wasije kujuta baadaye.

Kulingana na Burale mitandao ya kijamii ni zana nzuri ikiwa inatumiwa vizuri lakini pia ni zana mbaya wakati inatumiwa vibaya.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Churchill, Burale alishiriki:

"Uongo mkubwa wa kizazi hiki ni mitandao ya kijamii.Unakuta mtuamepatwa na msongo wa mawazo kwa sababu rafiki yake alipakia picha akiwa na gari la aina ya Rangre Rover

Kile ambacho mtu anaweza asijue ni kwamba yule mtu anaweza kuwa amemlipa mlinzi ili kumwonya wakati mmiliki wa Range Rover atakapofika.

Uhitaji wa kushindana ni mwingi sana. " Alizungumza Burale.

Aliongeza;

"Watu wengi wanacheza kwa mapigo ya jirani lakini kwaya yao imepoteza kipigo,unaishi kwa mafanikio ya watu wengine na hawajali

Baadhi ya watu wanaokushtua ndio hao hao watakaokusulubisha

Furahiya mitandao ya kijamii lakini usichukulie kwa uzitoUkitumia mitandao ya kijamii vizuri itakusaidia lakini usipofanya hivyo inaweza kukuharibia. "