'Sisi sio marafiki' Vera Sidika azungumzia uhusiano na Otile Brown, asema amefunga ndoa kihalali na Mauzo

Mwanasoshalaiti huyo pia amefichua kuwa walipatana na Mauzo kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita kwa wakati huo akiwa kwa uhusiano mwingine.

Muhtasari

•Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa hawana uhusiano wowote wa kirafiki na mwanamuziki Otile Brown

• Kwa sasa mwanasoshalaiti huyo ambaye ana ujauzito wa miezi sita ameweka wazi kuwa amefunga ndoa kihalali na kipenzi chake cha sasa Brown Mauzo.

VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti na mwanabiashara mashuhuri nchini Vera Sidika amepuuzilia mbali urafiki na aliyekuwa mpenzi wake Otile Brown.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa hawana uhusiano wowote wa kirafiki na mwanamuziki huyo

"Sisi sio marafiki" Vera alimjibu shabiki wake mmoja.

Wawili hao walichumbiana kwa kipindi kifupi na kutengana katika hali tatanishi mwaka wa 2018.

Kwa wakati huo wawili hao walionekana kupendana sana kilele cha mapenzi kikiwa Otile Brown kumtungia wimbo 'Baby Love' ambao ulielezea mapenzi yake kwa mwanasoshalaiti huyo.. 

Walipotengana Vera alishangaza wanamitandao baada ya kufichua hadharani kwamba Otile hakuwa anamtosheleza kitandani.

 Kwa sasa mwanasoshalaiti huyo ambaye ana ujauzito wa miezi sita ameweka wazi kuwa amefunga ndoa kihalali na kipenzi chake cha sasa Brown Mauzo.

Hata hivyo, Vera amesema kuwa hawajafanya harusi na mwanamuziki huyo ila watafanya sherehe hiyo wakati watakuwa tayari.

"Ikiwa wazungumzia harusi ambayo inahusisha mimi kuvaa gauni nyeupe na  bae akiwa amevalia suti n.k, basi hatujafanya hilo bado. Kuolewa kihalali, ndio tumeoana. Tutakapokuwa tayari tutafanya harusi jukwani, chakula, keki na hayo yote mengine. Hamna haraka" Vera alimjibu shabiki mwingine.

Mwanasoshalaiti huyo pia amefichua kuwa walipatana na Mauzo kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita kwa wakati huo akiwa kwa uhusiano mwingine.

"Tulipatana miaka miwili iliyopita katika hali ya kawaida tu na kusalimiana. Nilikuwa kwenye mahussiano mengine kwa wakati huo. Tena mwaka ulioita tukapatana tena Mombasa. Sikuwa na wig, sikuwa nimejipondoa na nilikuwa nimevalia dera. Nilikuwa nafanya kazi ya kutengeneza spa yangu mwezi Agosti" Vera alisema.

Vera amesema kuwa Mauzo alimpeleka kuona wazazi wake kitambo sana hata kabla wafunge ndoa.