(+Video) Vanessa Mdee apewa zawadi ya gari aina ya Range Rover 2021 na kipenzi chake Rotimi

Vanessa alijulisha mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia video fupi akiwa ndani ya gari lile huku ameshika ufunguo wa gari

Muhtasari

•Wapenzi hao wawili wameendelea kufurahia mapenzi yao yanayoonekana kuwa yamenoga kweli na kusherehekeana kila uchao.

•Rotimi ambaye ni mwigizaji mashuhuri Marekani alimnunulia Mdee zawadi ya gari aina ya Range Rover 2021 na kumkabidhi siku ya Jumatatu.

Vanessa Mdee na Rotimi
Vanessa Mdee na Rotimi
Image: INSTAGRAM// VANESSA MDEE

Mwanamuziki Vanessa Mdee kutoka Bongo na mpenzi wake Rotimi wameendelea kuonyesha dunia maana ya mapenzi halisi siku moja baada ya nyingine.

Wapenzi hao wawili wameendelea kufurahia mapenzi yao yanayoonekana kuwa yamenoga kweli na kusherehekeana kila uchao.

Rotimi ambaye ni mwigizaji mashuhuri Marekani alimnunulia Mdee zawadi ya gari aina ya Range Rover 2021 na kumkabidhi siku ya Jumatatu.

Vanessa alijulisha mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia video fupi akiwa ndani ya gari lile huku ameshika ufunguo wa gari.

Mwanamuziki huyo aliambatanisha video hiyo na wimbo 'Hakuna Mungu kama wewe'  na kuandika ujumbe ulioonyesha furaha yake.

"Mungu mkuu.. Anapokukabidhi ufunguo wa gari yako mpya aina ya 2021 Range" Vanessa aliandika.

Kwa upande wake Rotimi alimshukuru Mungu na mpenzi wake Mdee kwa kumuunga mkono katika kazi zake na kusema kuwa fanikio hilo limetokana na kufanya kazi kwa bidii na kuwa mwaminifu kwa Mola.

"Hili ni zao la kuepuka vikwazo, Hili ni zao la kufanya kazi kama inavyostahili. Hili ni zao la kutengeneza sanaa bora k.v muziki, kuwa mtu mwema, Mungu na kuwa mwaminifu, hili ni zao la kufanya yale ulisema utafanya na najisherehekea pamoja na timu yangu na mke wangu tumefaulu" Rotimi alisema.

Hivi karibuni Mdee alionyesha upendo mkubwa anao kwa kipenzi chake Rotimi kwa kuchorwa tatoo ya jina lake.

Mdee alifichua hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kupakia picha iliyoonyesha tatoo yake mpya ambayo ni jina Rotimi, jina ambalo mpenzi wake anatumia kwenye usanii wake.

Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2019 baada ya Vanessa kutengana na aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi kirefu, mwanamuziki Jux.