Vera Sidika adai kuwa uhusiano wake wa sasa na Brown Mauzo ndio mrefu zaidi maishani mwake

Vera Sidika amefichua kuwa kamwe hajawahi kuchumbia mwanaume mmoja kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja hapo awali.

Muhtasari

•Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa maishani mwake hajawahi kujiendekeza wa kwanza  kwa mwanaume yeyote

•Vera pia alifichua kuwa kabla apatane na Mauzo alikuwa hana mchumba kwa kipindi cha takriban  miezi tisa

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera Sidika amefichua kuwa kamwe hajawahi kuchumbia mwanaume mmoja kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja hapo awali.

Katika kipindi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanasoshalaiti huyo amasema kuwa uhusiano wake wa sasa na mwanamuziki Brown Mauzo ndio mrefu zaidi ashawahi kuwa ndani yake.

"Imekuwa baraka. Ndio uhusiano mrefu zaidi. Mwaka mmoja sasa" Vera alisema

Wawili hao walianza kuchumbiana hapo katikati mwa mwaka uliopita.

 Vera alikuwa akimjibu shabiki mmoja aliyetaka kujua kati yake na Mauzo ni nani alijipendekeza kwa mwingine wa kwanza.

Mama huyo mtarajiwa amesema kuwa maishani mwake hajawahi kujiendekeza wa kwanza  kwa mwanaume yeyote.

"Sijawahi kuwa wa kwanza kujipendekeza kwa mwanaume maishani mwangu. Mume wangu alikuwa wa kwanza kuja na alijua kabisa alichotaka. Huwa wanasema kuwa mwanaume hujua anachotaka na hawatapoteza wakati wowote wakikiona. Kweli alijipendekeza, tukafunga ndoa na sasa tunaanza familia ndogo" Alisema Sidika.

Mwanasoshalaiti huyo aliwacheka waliokuwa wakimkejeli kuwa kila mwaka alikuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa na mwanaume tofauti.

"Basi maadhimisho ya siku yangu ni mwezi ujao na bado niko na mwanaume yuleyule tu mmoja" Alisema huku akiambatanisha na emoji za kicheko.

Vera pia alifichua kuwa kabla apatane na Mauzo alikuwa hana mchumba kwa kipindi cha takriban  miezi tisa. Alisema kuwa kwa wakati huo hakuwa akisumbuliwa na  kumbukumbu zozote za uhusiano wake wa hapo awali.