Diamond na Hamisa Mobetto waadhimisha siku ya kuzaliwa ya mwana wao 'Simba mdogo'

Dylan ambaye ni mtoto wa tatu wa Diamond anayejulikana alikuwa anaadhimisha miaka minne tangu kuzaliwa.

Muhtasari

•Diamond almaarufu kama Simba alimsherehekea Dylan kwa ujumbe maalum kupitia ukurasa wake wa Instagram  siku ya Jumapili

•.Wikendi hiyo hiyo Diamond alisherehekea siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa binti wake  Latifah Dangote ambaye ni kifunguamimba wake pamoja na mwanasoshalaiti Zari Hassan kutoka Uganda

•Kando na Dylan na Tiffah, mwanamuziki huyo ana watoto wengine wawili ambao wanafahamika.

Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Diamond Platnumz na aliyekuwa mpenzi wake kwa wakati mmoja Hamisa Mobeto walisherehekea siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mtoto wao Dylan.

Diamond almaarufu kama Simba alimsherehekea Dylan kwa ujumbe maalum kupitia ukurasa wake wa Instagram  siku ya Jumapili.

"Ndio, simba mdogo alizaliwa siku kama ya leo" Aliandika Diamond.

Dylan ambaye ni mtoto wa tatu wa Diamond anayejulikana alikuwa anaadhimisha miaka minne tangu kuzaliwa.

Mamake Dylan, Hamisa Mobetto pia alimsherehekea mwanawe kwa jumbe maalum na kumuombea baraka za Mungu.

"Heri za kuzaliwa mwanangu Dylan. Nakupenda sana boouba. Mungu akulinde kwa ajili yangu." Mobetto aliandika.

Wanamitandao wengi ikiwemo wasani toka Kenya k.v Tanasha Donna, Diana Marua na Kate Actress(Selina) pia walituma jumbe zao za kumtakia Dylan heri za kuzaliwa.

Wikendi hiyo hiyo Diamond alisherehekea siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa binti wake  Latifah Dangote ambaye ni kifunguamimba wake pamoja na mwanasoshalaiti Zari Hassan kutoka Uganda.

"Heri ya kuzaliwa binti yangu mzuri na mzuri lovely @princess_tiffah 💝 .... maneno hayawezi kuelezea jinsi ninavyokupenda Miss World👸 .... siwezi subiri kusherehekea siku hii ya kuzaliwa na wewe, Jumamosi hii .... ❤🎂❤ @princess_tiffah ❤🎂❤," Aliandika Diamond.

Kupitia mazungumzo ya video kwa simu, Diamond aliahidi Tiffah kuwa angemfanyia sherhe kubwa ya kuadhimisha siku hiyo nchini Tanzania baada ya kukosa kuhudhuria sherehe iliyofanyika Afrika Kusini mnamo Jumamosi.

Kando na Dylan na Tiffah, mwanamuziki huyo ana watoto wengine wawili ambao wanafahamika.

Simba ana mtoto mwingine pamoja na Zari kwa jina Prince Nillan na Naseeb Juniour ambaye walipata pamoja na mwanamuziki kutoka Kenya Tanasha Donna.

Hata hivyo inafahamika kuwa nyota huyo wa Bongo ana watoto wengine wawili ambao hawajawahi kutambulishwa.