Kabi wa Jesus aadhimisha siku ya kuzaliwa ya mkewe kwa ujumbe maalum

Kabi amesema kuwa Milly ambaye kwa sasa anafikisha miaka 28 ndiye zawadi kubwa ashawahi kupokea maishani mwake na kudai kuwa yeye ni baraka kwa wengi.

Muhtasari

•Msanii mashuhuri Peter Kabi almaarufu kama Kabi wa Jesus anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake Milly wa Jesus.

•Kabi amesema kuwa Milly ambaye kwa sasa anafikisha miaka 28 ndiye zawadi kubwa ashawahi kupokea maishani mwake na kudai kuwa yeye ni baraka kwa wengi.

Image: INSTAGRAM//KABI WA JESUS

Msanii mashuhuri Peter Kabi almaarufu kama Kabi wa Jesus anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake Milly wa Jesus.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kabi amemtakia mpenzi wake  heri za kuzaliwa kwa ujumbe maalum.

Kabi amesema kuwa Milly ambaye kwa sasa anafikisha miaka 28 ndiye zawadi kubwa ashawahi kupokea maishani mwake na kudai kuwa yeye ni baraka kwa wengi.

"Siku kama ya leo malkia alizaliwa, zawadi kubwa zaidi Mungu ashawahi nipa na baraka kwa wengi. Malkia wangu Milly wa Jesus unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa nakutakia baraka maishani. Naomba mwaka huu upokee neema kubwa zaidi. Naomba mwaka huu uweze kufanya mambo makubwa ambayo hujawahi kufanyamaishani, upate raha kwa lolote ufanyalo. Nakutakia mafanikio kwa kila ufanyalo maishani.

Nasema yeyote atakayejaribu kukulaani badala yake akubariki. Kila utakachoguza  kistawi na zawadi ya wokovu maishani mwako ifikie wengi." Aliandika Kabi.

Mwanavlogu huyo aliwaomba masshabiki wake kumsaidia kumtakia mkewe heri za kuzaliwa.

Mamia ya mashabiki wamejumuika chini ya ujumbe wa Kabi kumtakia Milly heri za kuzaliwa na kutangaza baraka maishani mwake.