'Kama hujui kuomba slayqueen polepole enda ulale' Sonko ashauri 'sponsors' kuepuka vurugu dhidi ya wanawake

Sonko amewashauri wanaume hao kuwa wapole wanapojitetea kwa wasichana na kuepuka vurugu

Muhtasari

•Kupitia mtandao wa Facebook matendo ya kikatili yamekithiri miongoni mwa wazee tajiri  wanaochumbia wasichana wadogo almaarufu kama 'sponsors'.

•Mwasiasa huyo alikuwa anatoa hisia zake kuhusiana na video ambayo imeenezwa sana mitandaoni ikionyesha mwanamke mdogo akizozana na anayedaiwa kuwa 'sponsor' wake.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amekashifu matendo ya vurugu dhidi ya wanawake yanayotekelezwa na 'sponsors' 

Kupitia mtandao wa Facebook matendo ya vurugu yamekithiri miongoni mwa wazee tajiri  wanaochumbia wasichana wadogo almaarufu kama 'sponsors'.

Sonko amewashauri wanaume hao kuwa wapole wanapojitetea kwa wasichana na kuepuka vurugu.

"Siku hizi sponsors wamekithiri sana. Kama hujui kuomba slayqueen polepole acha kukunywa enda ulale" Sonko alisema.

Mwasiasa huyo ambaye pia ni mwanabiashara mahiri alikuwa anatoa hisia zake kuhusiana na video ambayo imeenezwa sana mitandaoni ikionyesha mwanamke mdogo akizozana na anayedaiwa kuwa 'sponsor' wake.

Wawili hao wanaonekana wakiwa wamekaa kwenye baa kisha ghafla bin vu 'sponsor' anageuka kuwa mkatili kwa msichana yule.

Hali inabadilika wakati mwanamke huyo anamkaza 'sponsor' kumgusa. Mzee huyo anaonekana kumshika msichana yule shingo na kumlaza kwa kiti.

"Kuna wakati wa urafiki na wakati wa biashara. Hii ni biashara! Unaskia?! Hii ni biashara... nishalipia! Kwenda huko." Mwanaume huyo anasikika akisema.

Msichana huyo ambaye anaonekana kushtuka kutokana na kilichokuwa kinaendelea anaangua kilio papo hapo.

Tazama video hapa:-

Kwenye ujumbe wake Sonko amemwelekeza msichana huyo kufika katika kituo cha polisi akachukue P3 na kumwahidi kuwa angemsaidia katika kesi yake.

"Sina kazi kwa sasa hebu huyu msichana achukue P3 anitafute tuinue huyu shoga" Sonko aliandika.