'Ukifika bunge bajeti ya michezo iongezwe' Ghost amsihi Jalango anayetazamia kuwa mbunge wa Lang'ata

Ghost alimwambia Jalang'o kuwa atakachotaka yeye sio zabuni ila angependa tu apeleke hoja bungeni kuwa bajeti ya michezo iongezwe ili vijana wasaidike.

Muhtasari

•Kwenye video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram Jumatano asubuhi, Ghost alimwambia Jalango kuwa ana maono kuwa atanyakua kiti cha ubunge cha  Langata mwaka ujao.

•Mtangazaji na mchekeshaji Jalango tayari ametangaza azma yake kuwania kiti cha ubunge cha Lang'ata ambacho kwa sasa kimekaliwa na Nixon Korir wa Jubilee

Image: HISANI

Mtangazaiji Jacob 'Ghost' Mulee na ambaye ni kocha wa Harambee Stars amesihi Jalang'o kutetea wizara ya michezo kuongezwa fedha.

Kwenye video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram Jumatano asubuhi, Ghost alimwambia Jalango kuwa ana maono kuwa atanyakua kiti cha ubunge cha  Langata mwaka ujao.

Ghost alimwambia Jalang'o kuwa atakachotaka yeye sio zabuni ila angependa tu apeleke hoja bungeni kuwa bajeti ya michezo iongezwe ili vijana wasaidike.

"Najua utakuwa mbunge 2022. Hayo ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu, sisi huwa na maono. Ukiingia kwenye baraza la mawaziri tayari utapewa wizara. Jalas mimi sitaki zabuni, nataka tu nikuja kwa wizara tuongee vile tunaweza kusaidia vijana ukifika bunge bajeti ya michezo iongezwe " Ghost aliambia Jalango.

Mtangazaji na mchekeshaji Jalango tayari ametangaza azma yake kuwania kiti cha ubunge cha Lang'ata ambacho kwa sasa kimekaliwa na Nixon Korir wa Jubilee.

Mwezi uliopita Jalango alijiunga rasmi na chama cha ODM kwenye matayarisho yake  ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.