'Ilianza kuwa sumu' Aliyekuwa mpenzi wa Karen Nyamu azungumzia uhusiano wao, alivyoambia Samidoh walipopatana

Saint alisema kuwa walipatana na staa huyo wa muguthi katika sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya binti yake na Karen na wakawa na mazungumzo mafupi.

Muhtasari

•Alipokuwa kwenye mahojiano na Alibaba katika kipindi cha Bustani, mcheza santuri huyo alisema kuwa walipatana na Karen kabla hajapata umaarufu mkubwa.

•Saint alisema kuwa Karen alitofautiana naye kuhusu mambo mingi ya kimaisha na baada ya hali ile kukithiri wakaonelea heri watengane kila mmoja aende njia tofauti.

•Mcheza santuri huyo alisema kuwa amewahi kupata na mpenzi wa Karen wa sasa na baba wa mtoto wake wa pili mwanamuziki mashuhuri Samuel Muchoki almaarufu kama Samidoh.

DJ Saint, Karen Nyamu, Samidoh
DJ Saint, Karen Nyamu, Samidoh
Image: RADIO JAMBO// INSTAGRAM

Aliyekuwa mpenzi wa wakili na mwanasiasa Karen Nyamu na ambaye ni baba wa mtoto wake wa kwanza, Jeremy Kevinsky almaarufu kama DJ Saint amefunguka kuhusu maisha ya uhusiano wao hapo awali na hali ilivyo sasa.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Alibaba katika kipindi cha Bustani, mcheza santuri huyo alisema kuwa walipatana na Karen kabla hajapata umaarufu mkubwa.

"Tulipatana naye hata kabla hajajiingiza kwenye siasa. Kwa wakati huo yeye alikuwa wakili tu nami nilikuwa nacheza santuri kwa hafla aliyohudhuria" Saint alisema.

Baada ya kujuana wawili hao walichumbiana kwa kipindi cha miaka kadhaa na hata kubarikiwa na binti pamoja.

Hata hivyo, uhusiano wao haukudumu  kwa kile baba huyo wa watoto wawili alisema kuwa 'uhusiano sumu'

Saint alisema kuwa Karen alitofautiana naye kuhusu mambo mingi ya kimaisha na baada ya hali ile kukithiri wakaonelea heri watengane kila mmoja aende njia tofauti.

"Ili niamue kwenda tulikuwa tumefikia hatua ambapo hatungerudi nyuma. Kila wakati tulikuwa tukizozana  na sikuona ikiwa vyema kulea mtoto katika mazingira kama yale. Hapo nikaona nimpatie nafasi yake nami  niwe na nafasi yangu. Hatua ile ilifanya kazi vizuri kwani uhusiano wetu ulikuwa umeanza kuwa sumu. Kila siku ilikuwa vita tu" Saint alisimulia.

Hata hivyo alieleza kuwa hawakukatiza mazungumzo yao na kwa sasa wao ni marafiki na wanashirikiana katika ulezi wa binti yao.

"Yeye ni mama mzuri sana kwa mtoto wangu" Alisema.

Saint alifichua kuwa Karen humfahamisha kila anapojitosa kwenye mahusiano mapya.

"Lazima ataniambia kwa sababu kama kuna mtu anakuja kwa ile nyumba pia mtoto wangu anahusika. Huwa ananimbia  akipata mpenzi anayekuja kwa nyumba yake" Saint aliendelea kusema.

Mcheza santuri huyo alisema kuwa amewahi kupata na mpenzi wa Karen wa sasa na baba wa mtoto wake wa pili mwanamuziki mashuhuri Samuel Muchoki almaarufu kama Samidoh.

Saint alisema kuwa walipatana  na staa huyo wa muguthi katika sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya binti yake na Karen na wakawa na mazungumzo mafupi.

"Niliambia Karen kwa kuwa hatuna ugomvi ningependa kujua kipenzi chake.. Samidoh akaja kwa sherehe na nikamkaribisha, tukapata kinywaji pamoja kisha nikamuita aje nikamwambia kuwa akiwa na uhusiano mzuri na mtoto wangu hatungekuwa na shida ila iwapo angekuwa mkatili kwake tungekosana" Alisema DJ Saint.

Alisema kuwa Samidoh alimhakikishia kuwa angekuwa mwema kwa mtoto wake kwa muwa pia yeye ni mzazi.

Saint hata hivyo alisema kuwa hana ufahamu wowote kuhusu uhusiano wa Karen na Samidoh kwa sasa kwani huwa hawazungumzi kuhusiana na hayo.