"Hawa watachomwa na Mungu" Mike Sonko awalaani vikali wapenzi wa jinsia moja

Mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na vituko amesema kuwa hata Mola hakubaliani na kitendo hicho.

Muhtasari

•Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike  Sonko ameonyesha kutokubaliana kwake na ndoa kati ya watu wa jinsia moja.

•Baadhi ya wanamitandao walitoa hisia zao pia wengine wakimuunga mkono huko kikundi kingine kikimkashifu kufuatia na matamshi yake.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike  Sonko ameonyesha kutokubaliana kwake na ndoa kati ya watu wa jinsia moja.

Mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na vituko amesema kuwa hata Mola hakubaliani na kitendo hicho.

Akitoa hisia zake mtandaoni Facebook kuhusiana na video iliyoonyesha mwanaume mmoja akiwa amepiga goti huku anamvisha mwenzake, Sonko alisema kuwa wawili hao wangepokea adhabu kali kutoka kwa Mungu.

"Hawa watachomwa na Mungu mpaka mik*nd* zao ziwe kama mboga ya mkunde" Sonko alisema. 

Baadhi ya wanamitandao walitoa hisia zao pia wengine wakimuunga mkono huko kikundi kingine kikimkashifu kufuatia na matamshi yake.

"Naamini kuwa ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke, lakini wacha Mungu awahukumu kwani ni watoto wake. Kutunza wanawake sio rahisi siku hizi" Jamaa kwa jina Jackson Wachira aliandika.

"Nani atatuoa kama hivi ndivyo hali ilivyo?" Mwanadada kwa jiana Exnovia Shantel alieleza hofu yake.

"Haya ni mawazo ya aina gani? Tunaishi katika dunia huru. Mwelekeo wa mapenzi una shida gani. Wacha wafurahie. Kama unaweza kuthibisha kuwa Mungu ni mwanaume basi kwa kweli watachomwa. Hongera kwao" Pety Nila aliandika

Soma baadhi ya maoni ya Wakenya hapa:-

Hawa watachomwa na Mungu mpaka mikunde zao ziwe kama mboga ya mkunde

Posted by Mike Sonko. on Friday, August 13, 2021

Je, hisia zako ni zipi kuhusu ndoa  kati ya watu wa jinsia moja.