'Nina deni la Mungu na watoto wangu tu,'Nicah The Queen awaonya wenye chuki

Muhtasari
  • Nicah The Queen awaonya wenye chuki,Aliweka wazi kwamba mtu ambaye ana deni lake ni Mungu na watoto wake
Nicah the Queen
Image: Studio

Msanii Nicah the Queen, ameaonya wakosoaji wake ambao wamekuwa wakisema mabaya tu kumhusu.

Kulingana na msanii huyo wakati maisha yake yalipokuwa yanaenda mrama hamna mkosoaji yeyote ambaye alikuwa anaonekana lakini wakati maisha yake yamerudi sawa wote wamejaa kumkosoa.

Aliweka wazi kwamba mtu ambaye ana deni lake ni Mungu na watoto wake.

"Wakati nilikuwa nikipitia njia ngumu maishani mwangu sikuwahi kukuona yeyote kati yenu zaidi haswa wale ambao huwa mnatuma vibes hasi kwenye ukuta wangu !!

Lakini sasa nimejipata mwenyewe na watoto wangu kurudi kwenye njia na kuishi kwa njia bora ninavyojua na nyote mnajaribu kuniangusha na maoni na maneno yenu mabaya ... mtu pekee anayenidai ni Mungu wangu na watoto wangu pekee!" Aliandika.

Pia Nicah alisema kwamba watu mashuhuri hupitia mambo magumu maishani mwao, ambayo mashabiki wao hawayafahamu.

"Kwa hivyo ikiwa huna kitu chanya cha kusema au kuunga mkono miradi yangu basi nyamaza !! Watu mashuhuri hupitia mengi nyuma ya pazia na unaweza kuwa sababu ya mtu kutarajia kuishi siku inayofuata au kumaliza yote !! Sisi pia ni BINADAMU na damu inaendesha kwenye mishipa yetu !!"