Akothee awasuta wakenya wanaokejeli Alfred Mutua na mkewe baada ya kutengana

Muhtasari
  • Akothee awasuta wakenya wanaokejeli Alfred Mutua na mkewe baada ya kutengana
Esther Akoth

Msanii Akothee, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewasuta wakenya ambao wanawakejeli Alfre Mutua na aliyekuwa mkewe Lilian Ng'ang'a baada ya kutengana.

Mutua na mkewe walivuma sana siku ya Jumapili, baada ya mkewe kutangaza kutengana kwao.

Pia amewaambia wakenya kama hawajawahi kuwa katika ndoa waache kunyoosha mikono yao na kumlaumu gavana huyo.

"Ikiwa haujawahi kuolewa, wacha kunyoosha kidole cha lawama 💪 kuangalia watu katika mahusiano mengi, mahusiano yasiyofaa, ndoa zilizovunjika lakini bado zinaendelea kwa ajili ya jamii, kuhukumu kuvunja 

👉bundles ni za bei nafuu, kuandika ni ya bei nafuu, kuadhimisha changamoto ni ya bei nafuu na rahisi zaidi, ni jinsi gani uhusiano wako unavyoenda au unakuchukua sasa? .

Dunia hii imeoza, hata kusherehekea kuanguka kwako kwa kaburi 🤔.Watu wale ambao hawajawahi kukujulia hali  wakati ukiwa hai, watakuja kuchukua picha na jeneza lako," Aliandika Akothee.

Baadhi ya wanamitandao na wakenya kupitia mitandaoni waliwakejeli Gavana Mutua na MKewe  na hata kuanza kutengeneza memes za kejeli.

"Kuangalia watu katika mahusiano mengi, mahusiano yasiyofaa, ndoa zilizovunjika lakini bado wako pamoja kwa ajili ya jamii, wanahukumiwa kuvunja kwa gavana & mke wake .🤔 👉wengine hajawahi hata kujaribu kuishi na mendelakini wana picha nyingi za ushahidi, achaneni na ndoa,"