Wino wa upendo! Kando na Mauzo, fahamu baadhi ya wasanii waliowahi kuchorwa majina ya wapenzi wao

Mauzo alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo kufuatia mapenzi makubwa anayo kwa mke wake.

Muhtasari

•Mauzo sio msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuchorwa jina la mpenzi wake mwilini. Kunao baadhi ya watu mashuhuri ambao wamechukua hatua kama ile hivi karibuni

Image: INSTAGRAM// BROWN MAUZO

Siku ya Jumatatu ulimwengu wa burudani ulipokea habari za kushangaza kwamba mume wa mwanasosshalaiti Vera Sidika aliamua kuchora jina lake mwilini kwa wino wa kudumu.

Mwanamuziki Brown Mauzo ambaye kwa sasa wamechumbiana na Vera kwa kipindi cha mwaka mmoja alichorwa jina la kipenzi chake kwenye mikono, karibu na makwapa

Hatua hiyo ilimuacha Vera katika hali ya mshangao na hakuweza kuzuilia furaha yake mitandaoni.

"Bae amechora tatoo ya jina langu. Hata sina la kusema. Brown Mauzo nakupenda" Vera aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mauzo alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo kufuatia mapenzi makubwa anayo kwa mke wake.

"Kwa ajili ya upendo wangu kwa mke wangu. Wangu wa pekee @queenveebosset" Mauzo alisema.

Mauzo sio msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kuchorwa jina la mpenzi wake mwilini. Kunao baadhi ya watu mashuhuri ambao wamechukua hatua kama ile hivi karibuni:-

1. Amber Ray

Image: HISANI

Uhusiano kati ya mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu kama Amber Ray nan mfanyibiashara  Jamal Marlow ulikuja kufahamika hadharani takriban miezi minne iliyopita.

Ingawa ndoa kati ya wawili hao imekabiliwa na misukosuko sio haba, mwanasoshalaiti huyo aliamua kupeleka mapenzi yao katika hatua nyingine na kuonyesha mpenziwe mapenzi makubwa anayo kwake baada ya kuchorwa jina lake mgongoni.

Amber Ray alifichulia wafuasi wake mitandaoni jina 'Marlow' ambalo lilikuwa limechorwa mgongoni mwake.

2. Vanessa Mdee

Mwezi uliopita, mwanamuziki kutoka Tanzania Vanessa Hau Mdee alionyesha upendo mkubwa anao kwa kipenzi chake Olurotimi Akinosho almaarufu kama Rotimi kwa kuchorwa tatoo ya jina lake.

Mdee alifichua hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kupakia picha iliyoonyesha tatoo yake mpya ambayo ni jina Rotimi, jina ambalo mpenzi wake anatumia kwenye usanii wake.

Wawili hao walianza kuchumbiana mwaka wa 2019 baada ya Vanessa kutengana na aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi kirefu, mwanamuziki Jux.

Harmonize na Paula Kajala

Fridah Kajala na Harmonize
Fridah Kajala na Harmonize
Image: HISANI

Mdee sio mwanamuziki wa kwanza kutoka Bongo ambaye amewahi kuchorwa jina la mpenzi wake.

Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake mwigizaji  Frida Kajala waliwahi kuchora herufi ya kwanza ya mwingine kwenye upande wa shingo zao .

Hata hivyo, Harmonize alifuta tatoo hiyo mwezi Aprili huku Fridah akificha yake pia wiki hivi karibuni baada ya kutengana.