(+Video) Bilionea mashuhuri Grand P arudiana na mpenzi wake mwanamitindo Eudoxie Yao

Eudoxie Yao alikuwa ametangaza kutengana kwao takriban wiki tatu zilizopita.

Muhtasari

•Grand P ambaye ni mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri nchini Guinea amepakia picha na video zao wawili ambazo zimeashiria kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa wamerudiana.

• Licha ya kuwa Grand P ni mtu mzima, ana mwili mdogo zaidi tofauti na watu wenye umri kama wake. Yao kwa upande wake ana mwili mkubwa kweli.

Image: INSTAGRAM// GRAND P

Baada ya kutangaza kutengana kwao wiki chache zilizopita, bilionea Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P kutoka Guinea wamerudiana tena na mpenzi wake mwanasoshalaiti Eudoxie Yao kutoka Ivory Coast.

Mwanasoshalaiti Yao ambaye amebarikiwa na makalio makubwa kweli alithibitisha kutengana kwao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii takriban wiki tatu zilizopita.

"Watu wangu, ni rasmi kuwa sina mchumba kwa sasa na sina nia ya kuchumbiana kwani nataka kuangazia muziki wangu. Kuweni na wikendi njema" Yao aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa mwezi Julai.

Hata hivyo, wiki chache baadae Grand P ambaye ni mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri nchini Guinea amepakia picha na video zao wawili ambazo zimeashiria kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa wamerudiana.

Siku chache zilizopita Grand P alipakia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amekamatwa na Yao na kuambatanisha na ujumbe mfupi wa mapenzi.

"Mapenzi ni kutunzana hata mkiwa mmekasirikiana. Nakupenda sana @eudoxieyao__ " Grand P aliandika.

Kuthibitisha zaidi kuwa waliokuwa wametengana kwa sasa wako pamoja tena, kwenye mtandao wa Facebook bwenyenye huyo ambaye ana maumbile ya kipekee alipakia video mbili zilizoonyesha akiwa ameandamana na mpenzi wake Eudoxie Yao wakielekea mahali palipoonekana kuwa hoteli.

"Mguu wako, mguu wangu" Grand P aliandika chini ya video hiyo.

Ton pied 🦶 mon pied 🦶 ❤️❤️❤️❤️

Posted by Grand P on Tuesday, August 17, 2021

Ndoa kati ya wasanii hao wawili aghalabu huwashangaza sana wengi kufuatia utofauti mkubwa wa kimaumbile kati yao. Licha ya kuwa Grand P ni mtu mzima, ana mwili mdogo zaidi tofauti na watu wenye umri kama wake. Yao kwa upande wake ana mwili mkubwa kweli.