Dada yangu alimuoa baba yangu wa kambo baada ya kifo cha mama yangu-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Kipusa asimulia sababu ya kukata tamaa ya kuolewa
sad woman
sad woman

Yote tumekuwa tukiyaona katika filamu, lakini kuna yale yanatendeka katika maisha ya wapendwa wetu.

Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na mwanamke mmoja aliyefahamika kama Paulina ambaye alinisimulia sababu yake ya kukata tamaa katika maisha ya ndoa.

Je sababu yake ni ipi?

"Baada ya kifo cha baba yangu mzazi mama yangu aliolewa na mwanamume mwingine ambaye alikuwa baba yangu wa kambo

Nilikata tamaa ya kuolewa, baada ya dada yangu kumuoa baba yetu wa kambo, hakujali kile jamii itasema wala kubeba laana, kwani walitoroka na baba yangu na kutacha na mama yangu

Ni jambo ambalo mama yangu hajapona hadi leo na ni kisa abacho kilitendeka miaka kumi iliyopita, huwa naona makovu ya mama yyangu machoni pake

Hatujawahi zungumza na dada yangu tangu atoroke na baba yangu wa kambo, ndio walikuwa wanapendana sana lakini si kudhani kwamba upendo wao utafika pale pa mume na mke

Huwa na muona dada yangu mitandaoni lakini hatuongei kwa sababu sijawahi msamehe kwa ajili ya kitendo ambacho alitutendea," Alieleza Paulina.

Je ni vyema mwanamke huyu kumsamehe dada yake na kuendelea na maisha yake au ushuari wako ni upi?