Mpenzi wangu aliniambukiza ukimwi akijua,na kuanza kunidhulumu-Mwanamke alia

Muhtasari
  • Kipusa asimulia yale alipitia mikononi mwa mpenzi wake baada ya kumuambukiza ukimwi
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Huku nje wanawake wanapitia mambo magumu kwani wanapata mateso kutoka kw wapenzi wao, huku wengi wakiambukizwa magonjwa.

Mwanamke mmoja amewaacha mashabiki wa Radiojambo, na majonzi baada ya kusimulia kile alipitia mikononi mwa mpenzi wake na baba ya mpenzi wake.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nina miaka 22 nilipatana na huyu mwanamume na akanioa, nilipokuwa kwao baba yake hakuwa ananipa heshima alikuwa pia ananichungulia nikioga nikiambia mtoto wake ananichapa

Tumebarikiwa na mtoto mmoja, na nina mimba nyingine,mtoto wangu amekuwa mgonjwa sana kumbe mume wangu alikuwa anatumia dawa kwa siri

Mwaka jana nilipokuwa naenda hospitalini kwa ajili ya ujauzio wangu wa pili,niliambiwa kwamba nina virusi vya ukimwi

Kumbe mpenzi wangu aliniambukiza akiwa anajua kwamba ana virusi vya ukimwi, alianza kunidhulumu akiingia nyumbani, baada ya kumuuliza kwa nini ameingia nyumbani usiku wa manane na akiwa amelewa

Sijui nifanye aje kwa maana amekataa kumlea mtoto wake na licha ya yote nina ujauzito mwingine na virusi vya ukimwi," Alieleza Mwanamke huyo.

Je ushauri wako ni upi kwa mwanamke huyu?