'Nataka nyumba ata kama ni ya mabati,'Mkewe Omosh aomba msaada wa kujengewa nyumba

Muhtasari
  • Mkewe Omosh aomba msaada wa kujengewa nyumba
  • Wakati huu, Bi Ngatia aliwaomba Wakenya kumsaidia kujenga nyumba ndogo ya chumba cha kulala, hata ikiwa imetengenezwa kwa mabati

Mke wa mchekeshaji Omosh, Bi Ngatia ameomba msaada kutoka kwa watu,wasamaria wema na wakenya kujenga nyumba.

Wenzi hao walihojiwa na Hiram Mainkwenye mitandao yake ya youtube ,ni kupitia papo hapo ambapo Omosh alilia msaada ya kuupokea kutoka kwa wakenya.

Wakati huu, Bi Ngatia aliwaomba Wakenya kumsaidia kujenga nyumba ndogo ya chumba cha kulala, hata ikiwa imetengenezwa kwa mabati.

Alielezea kuwa anaishi Kayole na watoto wake watatu, wote ambao ni watoto wa Omosh.

Kulingana naye, kumjengea nyumba hiyo kungemfanya hata kupata motisha zaidi ya kutafuta kazi na kupata pesa za kutosha kujijengea nyumba bora.

"Ikiwa nitapata nyumba, hata nyumba ya Mabati yenye chumba kimoja cha kulala ili nisijisumbue kulipa kodi huko Nairobi

Ninaomba hata nyumba ya Mabati, kwa sasa, ninaishi nyumba ya bedsitter ninalipa Ksh 5,000, "Bi Ngatia alisema.

Mama wa watoto watatu alisema kwamba maisha baada ya kuanza kwa janga la COVID-19 hayakuwa rahisi kwani kazyake ya uigizaji iliisha.

"Nilifurahi sana kufanya kazi Tahidi High. Nilikuwa nikilisha watoto wangu na kuwaelimisha kwa sababu ya kazi hiyo

Kisha COVID ilikuja, mimi na watoto wangu tukaanza kupata shida, tumefukuzwa nyumbani, watoto wamefukuzwa shule

Nilifukuzwa kutoka kwa nyumba, na mwenye nyumba akisema kuwa tuna pesa, na Omosh ana jina kubwa. Jambo hilo limeniathiri kisaikolojia najisikia kama kufunika uso wangu wakati wa kutembea. "

Haya yanajiri miezi chache bada ya Omosh kujengewa nyumba, na kisa kukamilika.