'Utakuwa moyoni mwangu milele,'Diana Marua amuomboleza nyanyake huku wakimpumzisha

Muhtasari
  • Diana Marua amuomboleza nyanyake huku wakimpumzisha
Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Siku chache zilizopita Diana Marua, alitangaza kifo cha nyanya yake, na kusema kwamba ni yeye alimlea na dada zake baada ya mama yake kuaga dunia wakiwa na umri wa chini.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Diana pia alifichua kwamba nyanya yake alikuwa amelazwa hpsitali kwa mwezi mmoja kabla ya kifo chake.

Siku ya JUmamosi ilikuwa ya huzuni kwa Diana  kwani walikuwa wanampumzisha nyanya yao.

Diana alieleza kuwa ndoto ya dadake mdogo kupata nafasi ya kumuona mamaye mara kwa mara haikutimia kwani aliangamia kutokana na maradhi ya kisukari takriban wiki tatu tu baada yake kujiunga na shule ya upili ya Moi

"Kipindi kifupi tu baada ya Michelle kujiunga na shule ya upili, sidhani hata alikuwa ametulia vizuri pale, takriban wiki mbili tatu hivi kwa bahati mbaya mamangu aliaga dunia .Alifariki baada ya kuugua kisukari kwa kipindi kifupi" Alisema Diana.

Huku akimuomboleza nyanya yake alimwambia kwamba atakuwa moyoni mwake milele.

"Tunakupumzisha siku hii ya leo shosh,asante kwa kunilea na kunifanya kuwa bora,utakuwa moyoni mwangu milele, nakusherehekea," Aliandika Diana.