Eric Omondi afichua itamgharimu mtu elfu 750,000 kuburudisha bila shati

Muhtasari
  • Eric Omondi afichua itamgharimu mtu elfu 750,000 kumburudisha bila shati
Eric Omondi
Image: Hisani

Mchekeshaji Eric OMondi, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua yatakayo mgharimu mtu kama anataka kuburudishwa naye bila shati.

Kulingana na Omondi, kukuburudisha akiwa amevalia shati itamgharimu mtu shillingi elfu 500,000, ilhali bila shati itamgharimu mtu elfu 750,000.

Omondi alishangaza Wakenya wengi mnamo Novemba mwaka jana wakati alionyesha mwili wake mpya wa misuli.

Mchekeshaji huyo amekuwa akivuma mara kwa mara mitandaoni, baada ya kipindi chake cha Wife material, na jinsi wamekuwa na ugomvi na aliyekuwa bosi wa KFCB Ezekiel Mutua.

"Kiwango vimerudi,kukuburdisha na shati ni elfu 500,000, na bila shati ni elfu 750,000," Aliandika Omondi.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya ujumbe wake Eric Omondi;

Githinji Robert Kimani: Another client is asking how much you charge if you don't come at all..

olesh81: Na bila suruali?

Smart Head: Huyu naye I thought alirudi majuu.Kumbe ako Nanyuki🥴

Collins Caleb: Chest gani? Are you going to install it before the show?