Mungu hakukuumba uwe 'Side chick'-Msanii Mercy Masika awaamba vipusa

Muhtasari
  • Msanii Mercy Masika awashauri wanawake,kuhusu kuwa mpango wa kando
Mercy Masika
Mercy Masika

Mercy Masika ni miongoni mwa wasanii wa nyimbo za injili ambao wameshikilia tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 5.

Masika alifahamika sana kupitia kwa kibao chake cha 'wema'.ambacho kilivuma sana kwenye mitandao ya kijamii.

Tabia ya kuwa mpango wa kando na kutafuta mpango wa kando zimezidi kuongezeka,na ndoa nyingi zimevunjika kwa ajili ya wenzi kutokuwa waaminifu.

Wakati au karne hii ya sasa unampata msichana mwenye umri wa chini, ana 'sponsor' ambaye ana umri wa baba yake.

Ni jambo ambalo limekuwa mtindo, na watu kutojali tamaduni za kabila na ndoa zao.

Masika amewashauri vipusa kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram kwamba hawakuumbwakuwa mipango ya kando.

Ni ujumbe abao ulipokelewa vyema na mashabiki huku wakikashifu wenye tabia hiyo;

"Mungu hakukuumba uwe side chick," Aliandika Mercy Masika.

Hizi hapa baadhi ya hisisa za wanamitandao;

call_me_ngendo: Leo ni kuambiana Ukweli .Baassss volume Iko Sawa

charleneniver: Amen, preach sis

wanjira_kamau: 🙌🙌🙌 highest form of belittling yourself! Preach!!

ambermaggie8: Wababa we are in this together

elly_andeyo: Scream this louder the devil out here telling women men are few and you need to be a second wife..

njokimuchira: Hallelujah, or even a second wife.