'Asante kwa kunihimiza,'Alfred Mutua amwandikia Lilian Ng'ang'a ujumbe baada ya kuhudhuria sherehe yake

Muhtasari
  • Alfred Mutua amwandikia Lilian Ng'ang'a ujumbe baada ya kuhudhuria sherehe yake

Jumatatu, Gavana wa Machakos Alfred Mutua aliandika ujumbe maalum kwa mkewe wa zamani Lillian Nganga, juu ya kile alichodai kama kumtia moyo kufanya sherehe yake ya kwanza ya kuzaliwa baada ya kutimiza miaka 51 .

Kwenye ujumbe wake aliouandika kupitia ukurasa wake wa twitter alimsifu Lilian.

ÔÇťAsante @ LillyanneNganga kwa kunitia moyo kuandaa sherehe yangu yakusherehekea siku yangu ya  kuzaliwa.

Ilikuwa ni sherehe yangu ya kwanza ya kuzaliwa na ilikuwa bora kuliko vile nilivyotarajia. Muziki, kampuni na mandhari ilikuwa ya kushangaza. Asante kwa marafiki wangu wote, matakwa mema na hali njema kutoka kwa watu wazuri," Mutua aliandika.

Jumapili, Gavana Mutua alifanya sherehe ya pamoja ya Kuzaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Next Level Music Rayvanny huko Emara Ole Sereni.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wanafamilia na marafiki wa karibu na hata wasanii.