'Tunakupenda,'Ujumbe wake Rosemary Odinga kwa mama yake anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Ujumbe wake Rosemary Odinga kwa mama yake anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa
Ida Odinga
Ida Odinga

Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Ida Odinga anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa hii lro,familia yake na wanamitandao walimwandikia jumbe za kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Binti yake mkubwa Rosemary Odinga alikuwa mtu wa kwanza kumtakia  mama yake heri njema siku yake ya kuzaliwa.

RoseMary alimwambia amam yake wanampenda.

"Heri njema siku yako ya kuzaliwa mama, tunakupenda," aliandika.

Siku hii maalum kwake, mama wa  watoto wanne amepokea upendo kutoka kwa mumewe, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

"Cha cha cha NyarOlwande; Happy birthday my dear," Raila aliandika.

Kitinda mimba wake  Ida, Raila Junior pia aliandika ujumbe wa kuzaliwakwa mama yake, na kumuombea Mungu amzidishie baraka.

"Chochote kinachofanya kujisikia furaha na kumpenda Mama, ndivyo ninavyotaka kwa wewe leo. Heri njema siku yako ya kuzaliwa Mama" Hebu Bwana awe pamoja nawe, kukukinga na kukulinda kwa uwepo Wake, "Raila Odinga Junior aliandika.

Ida Odinga aliolewa na Raila Odinga mwaka wa 1973 na pamoja wana watoto wanne, Fidel Odinga, Winnie Odinga Rosemary Odinga, na Raila Junior.

Mwaka jana Ida aliweka sherehe ya kipekee ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa nyumbani kwake Karen.

Ni sherehe ambayo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu,na baadhi ya wanasiasa.