Lala salama!Msanii Daddy Owen aomboleza kifo cha rafikiye aliyeaga kutokana na covid

Muhtasari
  • Pia alizungumzia hali ilivyokuwa ngumu kwake baada ya kupatikana na virusi vya corona
daddy owen
daddy owen

Mapema wiki hii msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen  aliweka wazi kwamba alipatikana na corona,lakini anaendelea vyema.

Pia alizungumzia hali ilivyokuwa ngumu kwake baada ya kupatikana na virusi vya corona.

Siku ya Jumatano, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram , alitangaza kifo cha rafiki yake ambaye aliaga kutokana na corona.

"Wiki iliyopita nilishiriki uzoefu wangu na covid na jinsi nilipona, naweza kumshukuru MUNGU πŸ™πŸΏ kwa bahati mbaya jana nilipoteza rafiki yangu mmoja ambaye hakuweza kupigana na virusi hivyo

sehemu ngumu zaidi ni kwamba tunaweza kuwa tumepata virusi wakati huo huo na sehemu ile ile

Kupokea na kukubali habari leo asubuhi ilikuwa moja ya mambo magumu zaidi ambayo nimekabiliana nayo mwaka huo

Kuiombea familia πŸ™πŸΏ itashiriki habari zaidi pamoja na picha tu wakati familia inashiriki kwanza na ikiwa nitapata idhini," Owen aliandika.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki wakimfariji Daddy Owen;

mercymasikamuguro: So sorry for the loss...wow we thank God he preserved you.

kalekyemumo: My deepest deepest condolences. May you find peace & comfort in God

classydripclosetke: Pole Sana to the family

paula_0490: Ooooh... so sorry for the lost😒

lizlenjo_kags: Poleni sana

iam_megan_jaymes: So so sorry my condolences πŸ’