(+Video)Alikiba abubujikwa na machozi baada ya kuona picha ya marehemu baba yake

Muhtasari
  • Alikiba abubujikwa na machozi baada ya kuona picha ya marehemu baba yake
Alikiba
Image: Alikiba/instagram

Msanii wa bongo kutoka Tanzania Ali Saleh Kiba maarufu Alikiba alivunja machozi baada ya shabiki kumshangaza na picha ya marehemu baba yake Mzee Saleh Kiba.

Hii ni baada ya msanii huyo kupakia video kwenye mitandao yake ya youtube,shaiki huyon akimtolea mchoro wa picha hiyo.

Kiba alijawa na hisia baada ya kuona picha ya baba yake marehemu, kitu ambacho hakuwa na matarajio.

Ali KIba kwenye ukrasa wake wa instagram alisema kuwa katika maisha alikuwa amepokea picha nyingi na uso wake lakini hakuwahi kufikiri kwamba shabiki atakwenda maili ya ziada na kumchora baba yake marehemu.

"Katika safari yangu ya muziki nimepata nafasi kusafiri sehem nyingi sana, nimekutana na mashabiki wengi wanaopenda muziki wangu mimi huwaita #Alikibloodfans, wao hunipa zawadi mbalimbali na moja ya zawadi kubwa nayopewa na wengi wao ni picha za kuchora kwa mkono nyingi zikiwa zangu, Nilipata zawadi hii kutoka kwa @ymakenya, alimchora Baba yangu mzazi ambaye hatuko nae tena duniani, ni kitu ambacho sikutegema wala kufikiria."

Msanii huyo alisema kwamba hiyo ni zawadi ya kipekee, ambayo amewahi pokea kutoka kwa mashabiki wake.

" !! Nashukuru sana kwa zawadi hii ambayo kwangu ni ya kipekee sana. Siku zote nitathamini na kushukuru kila mtu anaechukua muda wake kufanya kazi hii ya sanaa na kuonesha upendo kwangu !! Mwenyezi Mungu awazidishie baraka zake katika kazi zenuūüôŹūüŹŅ," Aliandika Kiba.

Mzee Mzee Saleh Kiba, alikufa mnamo Januari 17, 2019.

Picha hiyo ilitolewa na msanii wa Kenya kwa jina Ali Hassan. Ali amefahamu sanaa ya kuchora kwa kutumia penseli.

Hii hapa ideo hiyo;

The Official YouTube Channel Of Alikiba. Subscribe for the Latest Music Videos, Performances, and More.https://www.youtube.com/c/AlikibaOfficial Listen to Alikiba on: Audiomack: https://audiomack.com/alikiba Apple Music: https://music.apple.com/us/artist/alikiba/578354001 Boomplay: https://www.boomplay.com/share/artist/2051126 YouTube: https://www.youtube.com/c/AlikibaOfficial Spotify: https://open.spotify.com/artist/2nGoKcLdXktxEXvMdTDsIT Connect with Alikiba on Social Media: Instagram:https://Instagram.com/officialalikiba‚Äč Facebook:https://web.facebook.com/OfficialAlikiba‚Äč Twitter:https://twitter.com/officialAlikiba/‚Äč TikTok:https://vm.tiktok.com/ZSmuTQ2W/‚Äč Connect with Mayorkun on Social Media: Instagram:https://instagram.com/iammayorkun Facebook:https://web.facebook.com/mayorkunofficial Twitter:https://twitter.com/iammayorkun Website:http://mayorkun.com +For More Information Booking Alikiba: Contact:emailalikiba@gmail.com Manager:Aidancharlie1@gmail.com ¬©2021 Kings Music Records.All rights reserved.