Nikieleza jinsi ulivyoteka moyo wangu Lulu atahisi wivu-Ujumbe wake Rashid Abdalla kwa bintiye

Muhtasari
  • Ujumbe wake Rashid Abdalla kwa mwanawe
familia ya lulu hassan na rashid abdalla
familia ya lulu hassan na rashid abdalla

Mwanahabari Rashid Abdalla amemwandikia mwanawe ujumbe maalum anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Rashid amemsifia mwanawe na kumwambia kwamba aliuteka moyo wake siku alipozaliwa, na ni jambo ambalo mkewe atahisi wivu akilisikia.

Pia alimwambia kwamba ni baraka kwake maishani mwake, huku akisema kwama uwepo wake una nguzo muhimu maishani mwake.

Mwanangu Kiran nikianza kueleza jinsi ulivyo uteka moyo wangu kuanzia siku uliingia dunia kwa hakika @loulou_hassan atahisi wivu

Nikiamua kufafanua vipi wewe ni zaidi ya baraka kwangu bila shaka wakubwa zako Jibran na Irfan watahisi vibaya.

Laiti ntasimulia jinsi uwepo wako ulivyo nguzo muhimu kuu maishani mwangu itakuwa nongwa kwani waja pia hawatanielewa," Aliandika Rashid.

Alizidi na ujumbe wake, wa kushereheea na kumtakia mwanawe heri njema ya kuzaliwa.

"Kwa hivyo wacha kimya kimya nikutakie heri njema katika siku yako ya kuzaliwa. Mungu akujalie kuishi ukithamini watu kwa kujali utu

Nakuahidi ntaupambania urafiki wetu hudumu milele. Happy birthday Kikky ."