'Akaunti zenye jina langu ni bandia,'Edgar azungumza baada ya akaunti yake ya instagram kufutwa

Muhtasari
  • Edgar azungumza baada ya akaunti yake ya instaram kufutwa
b9c3ecdcf03a1db9270abfd631322c21-696x824
b9c3ecdcf03a1db9270abfd631322c21-696x824

Hivi karibuni akaunti ya instagram ya Edgar Obare ilipotea, hii ni baada ya kutoa na kufichuliwa kwa genge la wash wash.

Ambayo alifichua katika moja ya vlogs zake nyingi.

Kulingana na wanamitandao, inasemekana kwamba alizima akaunti yake kuwa salama kutokana na majina aliyoyataja.

Walakini hii sivyo ilivyo kwa sababu hivi karibuni Edgar alifichua kupitia akaunti zake zingine za mitandao ya kijamii kwamba akaunti yake imezimwa lakini hakutoa sababu za hiyo.

Alisema hata hivyo anafanya kazi bila kuchoka kupata akaunti yake kuu ya Instagram.

Alisema pia kuwa bado atakuwa akichapisha katika akaunti zake zingine za mitandao ya kijamii kabla ya akaunti yake kuu ya Instagram kutengenezwa au badala yake kurejeshwa.

"Akaunti yangu kuu ya instagram imefutwa,nafanya niwezalo ili kurejesha akunti yangu, wakati huo huo huwa tumejitayarisha kwa mambo kama hayo, 

Pia naweza kuwa nikipakia kwenye akunti hii," Aliasema Edgar.

Wakati huo huo mwanablogu huyo alisema kwamba akaunti ambazo zina jina lake sio zake kwa hivyo mashabiki wanapaswa kuchukua tahadhari hiyo.

"Akaunti zenye zina jina langu ni bandia, tafadhali ripoti."