Busu la mume wangu kila asubuhi lanitosha,'Vera Sidika afichua kwa nini huwapa watu 'Block' mitandaoni

Muhtasari
  • Vera Sidika afichua kwa nini huwapa watu 'Block' mitandaoni
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Vera Sidika amekuwa akivuma kwa muda, baada ya kufichua kwamba ana ujauzito wa msanii Brown Mauzo.

Kwa mujibu wa Sidika, alisema kwamba alishika mimba mapema mwaka huu mwezi wa Februari, siku ya wapendanao.

Mnamo Julai, 10 mwaka huu mwanasosholaiti huyo aliweka sherehe ya kufichua jinsia ya mwanawe.

Wiki jana Sidika alifichua na kusema kwamba atampa mwanawe kila atakacho.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Vera alifichua kwamba busu la mumewe Mauzo linamtosha.

Usemi wake unajiri baada ya baadhi ya wanamitandao kulaalamika kwamba ana wapa block watu ovyo.

Pia aliweka wazi kwamba huwa ana wapa watu 'block' baada ya kusema mambo ambayo hayastahili na hayamsaidii katika maisha yake.

"Watu kweli wana wazimu, siwezi wapa watu block kwa sababu ya kuto niuliza habari ya asubuhi,sijali ata kidogo

KItu cha kwanza mume wangu hufanya kila asubuhi katika maisha yake ni kunipa busu na kuniuliza habari ya asubuhi

Na hilo peke yake linanitosha kwa miaka kumi,huwa nawapa watu block kwa kuleta mambo ambayo hayastahili au hasi katika njia zangu

Huwezi kuwa unanitumia hadithi hasi kila wakati," Alisema Vera.

Aliwasuta wale wamekuwa akijifanya kwamba wanajali maisha yake ilhali wanafanya kinyume cha maneno yao.

"Hamna kitu ya maana unanitumia kunihusu, na unatarajia ni furahi juu ya hayo kisha unadai unajali kuhusu maisha yangu

Kwani wewe ni CNN ama KTN News ni lazima unitumie habari mbaya zikitendeka,habari njema hunitumii, zile mbaya tu ndio unatuma

Naona watu kwenye DM yangu wakiniambia kwamba mimi nina roho ndogo kwa kuma mtu block kwa sababu hakuniambia habari ya asubuhi

Na hao pia waekula block papo kwa hapo."