"Kila kitu ninachomiliki nilinunua na pesa na jasho langu" Tanasha Donna ajitenga mbali na biashara laghai ya 'Wash Wash'

Tanasha amewakashifu sana wale wanaomhusisha na biashara haramu na kuwapa onyo kali

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo amesema kuwa huo ni uvumi tu na kudai kuwa anayeueneza anatafuta umaarufu tu.

•Mama huyo wa mtoto mmoja amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii ili kupata mali yote anayomiliki kwa sasa.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Aliyekuwa mke wa Diamond Platnumz mwanamuziki Tanasha Donna kutoka Kenya amepuuzilia mbali madai kuwa anajihusisha na biashara laghai maarufu kama 'Wash Wash'

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, msanii huyo ambaye ni miongoni wa waliokuwa wakivuma mitandaoni baada ya kuhusishwa na biashara hiyo haramu amesema kuwa huo ni uvumi tu na kudai kuwa anayeueneza anatafuta umaarufu tu.

"Mimi sio wale wa kuzungumzia mambo lakini YO! Uvumi huu wote umezidi sasa. Mtu anawezaje kuamka siku moja na kuamoua kutengeneza habari za uongo ili tu apate umaarufu??" Tanasha aliandika.

Mama huyo wa mtoto mmoja amesema kuwa amekuwa akifanya kazi kwa bidii ili kupata mali yote anayomiliki kwa sasa.

Tanasha amewakashifu sana wale wanaomhusisha na biashara haramu na kuwapa onyo kali.

"Nafanya kazi kwa bidii kupata mali yangu! Kila kitu ninachomiliki leo nimenunua na pesa nilizofanyia kazi na jasho langu! Msitaje jina langu kwenye biashara zenu. Wengine wenu mnaumiza sana!!" Amesema Donna.

Tanasha ni miongoni wa wasanii ambao wamejitokeza kujitenga na biashara hiyo baada ya majina yao kutajwa. Wengine ambao wamepuuzilia mbali kuhusika ni pamoja na Betty Kyalo na Jalang'o.