'Single mothers'Elimisheni watoto wenu bila kulalamika,'Akothee asema baada ya mwanawe kufanya haya

Muhtasari
  • Akothee awashauri akina mama wawaelimisha watoto wao bila kulalamika
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Image: Instagram

Kama umekuwa mwanamitandao lazima uwe umepatana na akunti ya msanii Akothee, ambaye anafahamika kama 'President of single mothers'.

Akothee amekuwa akiwahimiza wazazi hasa wanawake wawasomeshe watoto wao, bila kulalamika.

Bila shaka Akothee ni miongoni mwa wasanii ambao wamekuwa wakiwapa watu ushauri na hata kupakia maisha yao mitandaoni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee alishiiki furaha yake  baada ya kifungua mimba wake kuwa mfano mwema.

Kulingana na msanii huyo Vesha amekuwa akimtumia pesa licha yake kujua kwamba haitaji pesa zozote.

Akothee amesema kwamba mwanawe amekuwa akifanya hayo kila mwisho wa mwezi, na kusema kwamba amefuata nyayo zake.

"Single mothers ELIMISHeni WATOTO WENU BILA KULALAMIKA πŸ’ͺ Ohh Mungu wangu nina furaha sana , niruhusu kushiriki hii na wewe 😭😭😭😭😭😭😭

Binti yangu VESHA AWUOR OKELLO Mkurugenzi wa AKOTHEE SAFARIS .ni mzaliwa wangu wa kwanza πŸ™ Alihitimu mwaka jana, na akapata kazi mara baada ya kuhitimu, Alitafuta kazi hiyo mwenyewe bila kunihusisha πŸ€”

Nilikuwa nikishughulika na ukarabati wa nyumba zangu na kujenga suti za jumba wakati alitangaza kuondoka kwake kwa kazi yake mpya katikati ya corona, Ilikuwa mshtuko kwangu, na haikutua vizuri

Ili kupunguza hadithi ndefu, Msichana huyu hunitumia pesa kila mwezi, wakati anapokea mshahara wake 😭😭😭😭😭😭😭😭, sijui kwanini anafanya hivi, kwa kadri anavyojua sihitaji pesaπŸ€”πŸ€”πŸ€”

Pia mimi nilikuwa natuma pesa kwa mama yangu hata wakati sikuwa na mengi, je!amefuata nyayo zangu? Au ni moyo wake tu πŸ™πŸ™πŸ™," Aliandika Akothee.

Vesha alihitimu mwaka jana, na kufanya sherehe ya kipekee iliyohudhuriwa na watu tofauti.